Katika
kuelekea sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga
kikamilifu kuhakikisha wakazi wa Mkoa wa Mbeya, wageni na wakazi wa
mikoa jirani wanasherehekea sikukuu hii kwa amani na utulivu.
Kwa
kutambua kuwa Mkoa wetu unapakana na nchi jirani ya Malawi pia barabara
kuu inayounganisha nchi yetu na nchi jirani pamoja na mikoa jirani
imepita hapa, tumejipanga vizuri kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa
barabara wakiwemo madereva na watembea kwa miguu.
Wito
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ni kwa watumiaji wote wa barabara
kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka
ajali zinazoweza kuepukika.
Sambamba
na hilo, tumejipanga vizuri kuhakikisha maeneo yeto tete kama vile
Mlima Nyoka, Mlima Iwambi, Mlima Igawilo na Mwansekwa ulinzi na usalama
umeimarishwa katika kipindi chote cha sikukuu ya Pasaka kama ilivyo kwa
siku nyingine.
Kuelekea
kipindi hiki cha sikukuu, waumini wa madhehebu ya Kikristu ushiriki
katika ibada/misa kwa nyakati tofauti kulingana na ratiba zao, Jeshi la
Polisi limejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama katika makanisa hasa
katika misa au ibada za mkesha.
Aidha
tunatoa wito kwa viongozi katika makanisa kuhakikisha wanaweka
utaratibu mzuri hasa katika suala la ulinzi kwa kuzitumia kamati za
ulinzi na usalama ili kuhakikisha ulinzi katika maeneo ya ndani na nje
ya makanisa hasa sehemu za maegesho ya magari panakuwa salama kabisa.
Pia
tunatoa rai kwa wamiliki wa kumbi za starehe kufuata sheria hasa
kuzingatia leseni zao za biashara zinavyowaelekeza ikiwa ni pamoja na
kuzingatia muda wa kufungua na kufunga sehemu zao za biashara, wenye
kumbi za muziki kuhakikisha kumbi zao zinaingiza idadi ya watu
inayohitajika [capacity] pamoja na kuweka walinzi katika maeneo
yanayowazunguka.
Kuelekea
msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, ni wito wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi na
usalama wa mtoto, pia kuwasaidia watoto kuwavusha katika maeneo tete
kama vile barabara au maeneo yenye mito ili kuepuka madhara yanayoweza
kuwapata.
Pia
ili kuepuka watoto kupotea katika kipindi hiki, wazazi na walezi
wanapaswa kuongeza umakini, uangalizi kwa watoto wao kila mahali
wanapokwenda iwe ni makanisani, misikitini au katika maeneo yenye
michezo ya watoto.
Pia
tunasitiza ulinzi na usalama katika makazi yetu, kuhakikisha kwa wale
wanaotoka kwenda katika misa au ibada za mkesha kuacha waangalizi pia
kuhakikisha tunajilinda kwa kufunga milango na madirisha ili kuepuka
uhalifu katika nyumba zetu.
Aidha
tunasisitiza utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu kupitia namba za
simu za viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kama ifuatavyo:-
RPC…………………………………………………………….0715 009 931
RCO [Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa]………0658 376 052
STAFF OFFICER [Msaidizi wa RPC]………………….……0658 376 006
OPERATION OFFICER [Mkuu wa Operesheni Mkoa]..…..0754 466 924
RTO [Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa]……0658 376 472
OC FFU [Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia]……..…….0658 376 009
OCD MBEYA………………………………………………….0659 884 996
OCD MBALIZI………………………………………………..0655 248 381
OCD CHUNYA………………………………………………..0782 746 543
OCD MBARALI……………………………………………....0659 885 948
OCD RUNGWE……………………………………………….0659 885 253
OCD KYELA………………………………………………….0659 887 919
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post A Comment: