MKUU Wa Wilaya ya Ilala , Mh Sophia Mjema, amewataka Watumishi wa Mahama ya Ilala kusimamia maadili wakati Wa kutoa hukumu za kesi kwa  Wananchi.


 Ameyasema hayo wakati Wa kikao cha Kamati ya Maadili ya Watumishi Wa Mahakama Wilaya ya Ilala kilichofanyika Leo kwenye Ofisi yake Ilala Jijini Dar es salaam.

 Akizungumza na Waandishi Wa Habari, DC Mjema, amesema madhumuni ya kikao hicho ili kuwa ni kupokea malalamiko yanayo mgusa Mtumish Wa Mahakama ili kuyafanyia kazi. Amesema kwamba kamati ya Maadili ya watumishi Wa Mahakama Wilaya ipo  kwa mujibu Wa Sheria ya Utawala Wa Mahakama ( Judicial Administration Act) 2011 kifungu namba 51.

Aidha DC Mjema amesema kwamba majukumu ya kamati ya Maadili yameainishwa katika kifungu cha 51 (3) (1) ambapo ni kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi kwa mujibu Wa Sheria hiyo pamoja na kufanya uchunguzi kuhusu utendaji Wa Mahakama za mwanzo na majukumu mengine. 

" Hiki ni kikao halali na kipo kwa mujibu Wa kisheria, niwaombe watumishi zingatieni sana Maadili hakikisheni kesi zote zinaendeshwa kwa Sheria bila uonevu wala viashiria vya rushwa mkifanya hivyo Wananchi Hawa watajenga imani kubwa na Mahakama yao  na kama mnavyofahamu awamu hii ya tano  sio ya kuchezea Mh Rais wetu Dr John Magufuli anataka haki na kusimamia wanyonge lindeni Maadili mtakuwa salama" Amesema DC Mjema.

DC Mjema amesema licha ya kukosekana kwa malala miko yanayomgusa Mtumish lakini yapo maeneo ambayo aliyabaini yenye malalamiko.

 Amesema miongoni mwa malalamiko ni pamoja na ucheleweshwaji Wa kesi mfano Rushwa, upatikanaji Wa nakala za hukumu Mahakama ya Buguruni na Ukonga, malalamiko ya vitendo vya rushwa, Lugha zisizoridhisha kutoka kwa baadhi ya watumishi Wa Mahakama na taarifa za majarada kupotea.

Hivyo DC Mjema amewata watumishi kubadilika na kuendana na kasi ya Mh Rais Dkt John Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza kesi zilizopo Mahakamani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: