Sunday, 31 March 2019

WAZIRI WA KILIMO AFUNGUA MKUTANO MKUU TFA

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima  Tanganyika Peter Sirikwa akizungumza katika mkutano mkuu wa TFA

Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga akizungumza katika mkutano mkuu wa TFA uliofanyika jijini Arusha
Viongozi wa TFA wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga


Na Vero Ignatus,Arusha.

Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga amefungua mkutano mkuu wa wanahisa wa Chama cha Wakulima la Tanganyika (TFA) kilichowakutanisha wadau wa kilimo na wanahisa kwa pamoja ili kujadili maendeleo ya kilimo
Hasunga ameipongeza TFA kwa juhudi wanazozifanya katika kukuza sekta ya kilimo nchini ambayo ni kiinua mgongo na imeajiri watu wengi zaidi ya asilimia 80% ya Watanzania.
Akizungumza katika mkutano huo ambao uliambatana na utoaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wakulima hao .
Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na TFA katika kutatua changamoto za wakulima ili kuboresha sekta ya kilimo.
Mwenyekiti wa Chama  cha Wakulima TFA Peter Sirikwa amesema kuwa TFA iko mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo ya kilimo nchini na kuwanganisha wadau wa kilimo kwa pamoja

No comments:

Post a comment