Monday, 4 March 2019

Wajapani watua Arumeru na teknolojia ya kuondoa madini ya Floraidi kwenye maji


Watalamu wabobezi wa tafiti na teknolijia ya kutibu maji, wametua katika halmashauri ya Arusha, kwa lengo la kuhawilisha teknolojia ya kutibu maji na kuondoa kiwango cha madini ya Floraidi kwa kutumia nyuzi za pamba, wakitokea chuo kikuu cha Shinshu cha nchini  Japani.
Wabobezi hao kutokea nchini Japani, wamepata fursa ya kukutana na kufanya mhadhara na wadau wa sekta ya maji, ndani na nje ya halmashauri hiyo, wenye lengo la kuwa na uelewa wa pamoja wa teknolojia mbalimbali za kutibu maji, mhadhara uliofanyika kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mdahalo huo, Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, ameelezea hali halisi ya upatikanaji wa maji katika mkoa wa Arusha, na kuthibitisha uwepo wa changamoto kubwa ya madini ya Floride kwenye maji ya ukanda huo.
Amesema kuwa, licha ya kuwa serikali imefanikiwa kusambaza maji vijijini kwa asilimia 63 mpaka sasa, lakini bado baadhi ya maeneo, kuna tatizo la uwepo wa kiwango kikubwa cha madini ya Floraidi kwenye maji kulinganisha na kiwango kinachofaa kwa binadamu kilichotolewa na Umoja wa Mataifa, madini ambayo yana madhara kwa bianadamu.
Kwitega afafanua kuwa, takwimu zinaonesha takribani asilimia 42 ya vyanzo vya maji katika mikoa ya Arusha, Shinyanga, Singida na Manyara, vimeathiriwa na uwepo wa madini ya Floraidi iliyozidi kiwango cha kimataifa kinachokubalika na Shirika la Afya Duniani cha miligramu 1.5 kwa lita.
Kutokana na takwimu hizo, Kwitega amesema, ni dhahiri kuwa miradi mingi ya ya maji iliyopo na inayoendelea kujengwa mijini na vijijini katika mikoa hiyo, inahitaji mifumo na miundo mbinu bora na rahisi ya kutibu maji na kuondoa kiwa cha madini hayo y a Floraidi kwa ajili ya usalama wa afya za wananchi.
Hata hivyo wajapani hao, wameelezea aina tofauti za teknolojia ya kutibu maji na kuondoa madini yote yasiyo rafiki kwenye maji, ikiwemo madini hatari ya Floraidi, teknolojia inatumia baadhi ya malighafi zinazopatikana hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Sayansi na Teknolojia nchini Japani, Profesa  Yoshiko Shirokizawa, Mlamu mbobezi wa masuala ya utafiti kutoka  chuo kikuu cha Shunshi cha nchini Japa, amesema kuwa, teknolojia hiyo ya kuondoa madini ya floraidi, inatumia nyuzi za pamba, malighafi ambayo inapatikata kwa wingi hapa Tanzania.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, amethibitisha uhutaji mkubwa waa teknolojia ya kuondoa madini ya floraidi kwenye maji katika halmashauri yake, kutokana na uwepo wa watu walioathirika na madini hayo katika kijiji cha Lemanda kata ya Oldonyosambu.
Aidha mkurugenzi Mahera amefafanua kuwa, teknolojia iliyoelekezwa na wajapani hao inaonekana ni nzuri japo kuwa bado ina uwezo wa kutibu maji kwa kiwango kidogo, wakati hitaji la  halmashauri kwa sasa ni teknolojia rahisi ya kuondoa madini hayo, kwa kutibibu kiasi kikubwa cha maji kwa wakati mmoja na kushauri kuwa, watalamu hao kutoka Japani kushirikiana na kituo cha kufanyia tafiti cha Tanzania na kufanya tafiti zaidi kwa pamoja ili kuweza kupata njia nzuri zaidi ya kuondoa madini ya floraidi iliyozidi kwenye maji kwa kutibu kiasi kikubwa cha maji.
Aidha amewataka wajapani hao kuwahusisha na kuendelea kutoa mafunzo zaidi kwa wadau na watalamu wa maji wa kitanzani juu ya uendeshaji wa teknolojia hiyo na kuwafanya kuifahamu zaidi teknolojia hiyo.

No comments:

Post a Comment