Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Ignas Rubaratuka akizungumza kwenye halfa ya makabidhiano ya mabati 379 yenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule ya sekondari ya Tanga ufundi (Tanga School) kwajili ya kumalizia nyumba 5 za walimu kama sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Magufuli za upatikanaji wa elimu bora mashuleni


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza wakati wa makabidhiano kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi
 Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano ya mabati 379 yenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule ya sekondari ya Tanga ufundi (Tanga School) kwajili ya kumalizia nyumba 5 za walimu kama sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Magufuli za upatikanaji wa elimu bora mashuleni.

 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko

 PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akieleza jambo wakati wa halfa ya makabidhiano ya mabati 379 yenye thamani ya shilingi milioni 15 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto katika shule ya sekondari ya Tanga ufundi (Tanga School) kwajili ya kumalizia nyumba 5 za walimu kama sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Magufuli za upatikanaji wa elimu bora mashuleni.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Ignas Rubaratuka kulia akimkabidhi mabati
379 yenye thamani ya shilingi milioni 15 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto katika shule ya sekondari ya Tanga ufundi (Tanga School) kwajili ya kumalizia nyumba 5 za walimu kama sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Magufuli za upatikanaji wa elimu bora mashuleni.
 Sehemu ya watumishi wa Bandari ya Tanga wakiwe kwenye Halfa ya makabidhiano ya mabati 379 yenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule ya sekondari ya Tanga ufundi (Tanga School) kwajili ya kumalizia nyumba 5 za walimu kama sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Magufuli za upatikanaji wa elimu bora mashuleni.
 Sehemu ya walimu wa shule ya Sekondari Tanga School wakiwa na wanafunzi wao wakishuhudia makabidhiano ya mabati 379 yenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule ya sekondari ya Tanga ufundi (Tanga School) kwajili ya kumalizia nyumba 5 za walimu kama sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Magufuli za upatikanaji wa elimu bora mashuleni.
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya mabati 379 yenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule ya sekondari ya Tanga ufundi (Tanga School) kwajili ya kumalizia nyumba 5 za walimu kama sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Magufuli za upatikanaji wa elimu bora mashuleni kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Ignas Rubaratuka kushoto  ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi



Mamlaka ya bandari Nchini (TPA) imekabidhi mabati 379 yenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule ya sekondari ya Tanga ufundi (Tanga School) kwajili ya kumalizia nyumba 5 za walimu kama sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Magufuli za upatikanaji wa elimu bora mashuleni.

Akikabidhi mabati hayo kwa uongozi wa shule hiyo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya bandari Tanzania Prof Ignas Rubaratuka alisema wao kama mamlaka ya bandari wameona ni vyema warushishe kwa jamii kile wanachokipata katika kusaidia katika Nyanja mbalimbali kwanjamii katika elimu, afya na maafa.

Alisema ili kuwa na elimu bora ni lazima kuwe na mazingira bora pamoja na mambo mengine muhimu yanayotakiwa hivyo wameona ni vyema wachangie katika kuboresha mazingira ya walimu kwani walimu ni sehemu muhimu katika kutoa elimu bora.

‘’Kwa shule hii leo tunatatoa mabati haya 379 yatakayosaidia kupaua nyumba 5 za walimu ambapo tunaamini kuwa yatasaidia kuboreshamazingira  ya  walimu  ambapo  watatoa  elimu  bora  kwa  wanafunzi mwetu  ambao  ndio  tegemeo  letu  la  taifa  ambazo  pia  watakuwa wafanyakazi  wetu  wa  bandari   kwa  baadae,”alibainisha Prof Ignas.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya bandari Tanzania Mhandisi Deusdedit Kakoko   alisema  kutokana na mapato kwenye bajeti wanaamua kuwarudishia  wananchi walipo karuibu na mazingira ya bandari hivyo kutokana na mapato wanayoyapata katika vipindi hivi vya miaka miwili wameendelea kufanikiwa kuanzia kwenye kuhudumia shehena kubwa zaidi kuliko kipindi cha nyuma.

Alisema kwenye mapato wanaamini bandari ndio taasisi pekee kati ya taasisi zote za Umma na binafsi ambayo inatoa mchango mkubwa kuliko mtu yeyote kwenye serikali hivyo ameeleza kuwa wakishapata mapato hayo wanawakumbuka wananchi ambao wanapohudumia meli nao hushiriki kufanya kazi pamoja.

Alisema kati ya bandari nyingi au maeneo yalipojengwa bandari wameweza kugawanya kwenye halmashauri na wilaya ambazo zinazunguka bandari kupata kile walichokipata ambapo kwa mwaka huu katika Mkoa wa Tanga wataweza kutoa vitu mbalimbali katika sehemu tofauti tofauti katika bajeti ya milioni 50 waliyoitenga ambapo wanatarajia kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Hospitali ya rufaa ya Bombo na kusaidia madawati katika Wilaya ya Pangani.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya uongozi wa shule hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliishukuru mamlaka ya bandari Tanzania kwa kutoa msaada huo na kuiomba mamlaka hiyo iendelee kutoa msaada shuleni hapo kwakuwa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu mibovu ya mfumo wa majitaka pamoja na uzio wa shule.

Mkuu huyo wa wilaya alisema mchango huo wa mabati utawasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo la nyumba za walimu na kuwaomba wasiishie hapo wanaendelee kumuunga mkono Rais Magufuli katika Nyanja mbalimbali.

‘’Ndani ya jiji la Tanga tuna mahitaji ya madarasa 71 ili wanafunzi
wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza waweze kwenda mashuleni kwani asilimi 87 ya jiji la Tanga wanafunzi wetu wamefaulu kasoro wanafunzi 13 tuu ndio waliofeli tuendelee kuunga mkono jitihadahizi,’’alibainisha DC Mwilapwa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Andrew Mwakanyamale aliishukuru mamlakahiyo ya bandari kwa msaada waliopatiwa na kusema kuwa msaada huo utasaidia kukarabati maeneo mbalimbali ya shule hiyo na hatimaye waweze kufanya vizuri katika shule hiyo aliyosoma Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete.

Mwisho.
Share To:

Post A Comment: