Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu (wa tatu kulia)  akipewa maelezo kutoka kwa mkazi wa eneo la kihisitoria la Mikindani, Said Halfani kuhusiana na kisima cha asili cha Haikata kilichopo tangu  mwaka 1545  ambacho hadi sasa  kina maji yanayotumiwa na wakazi wa eneo hilo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajilli ya kujionea kisima hicho ambacho ni moja ya kivutio cha utali katika eneo hilo la Mikindani mkoani Mtwara. Wenghine ni wananchi pamoja na watumishi wa mkoa huo
   Baadhi ya jengo la zamani la kihistoria la ambalo ni kivuto cha utalii ambapo Taasisi za Uhifadhi nchini zitakuwa na jukumu la kukarabati pamoja na kuyasimamia ili kuchagiza utalii.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu akioneshwa baadhi ya picha kutoka kwa Afisa wa Malikale a,mbaye ni mkuu wa Kituo cha Makumbusho ya Mikindani, Paul Ngahane wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea eneo la kihistoria la Mikindani liliopo katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kujionea maeneo ya kihistoria. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye bango la kisima cha asili cha Haikata kilichopo tangu  mwaka 1545 ambapo hadi hivi sasa  maji hayo yanaendelea kutumiwa na wakazi wa mji wa kihistoria wa Mikindani.
.Moja jengo la kihistoria ambalo  Taasisi za uhifadhi nchini zinatarajia kukayakarabati kwa ajili ya utalii wa kiutamaduni na khistoria.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu (wa tatu kulia)  akipewa maelezo kutoka kwa mkazi wa eneo la kihisitoria la Mikindani, Said Halfani kuhusiana na kisima cha asili cha Haikata kilichopo tangu  mwaka 1545  ambacho hadi sasa  kina maji yanayotumiwa na wakazi wa eneo hilo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajilli ya kujionea kisima hicho ambacho ni moja ya kivutio cha utali katika eneo hilo la Mikindani mkoani Mtwara. Wenghine ni wananchi pamoja na watumishi wa mkoa huo.

Serikali imeanza mkakati maalum wa kuinua Utalii wa kiutamaduni na wa kihistoria kwa kuvigawa vituo 16 vya Malikale  kwa Taasisi za uhifadhi nchini.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kupitia upya sera ya Malikale  ya namna ya  kuyahifadhi maeneo hayo kufuatia majengo mengi ya kale na ya kihistoria kuwa katika hali mbaya ya uchakavu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Mhe. Constantine Kanyasu alipotembelea mji wa kihistoria wa Mikindani katika Manispaa ya Mikindani,mkoani Mtwara ambao kwa sasa  eneo lake linasimamiwa na kuendeshwa na Taasisi ya  Makumbusho ya Taifa.

Amesema lengo la uamuzi huo ni kuziwezesha Taasisi zitakazokuwa na jukumu la usimamizi  ziyakarabati na kuyasimamia  maeneo hayo  ya kihistoria ili  yaweze kuchangia katika pato la Taifa kupitia sekta ya utalii nchini.

Mhe. Kanyasu amesema vituo hivyo 16 vitawekwa chini ya Hifadhi za Taifa(TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro(NCAA), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA), Makumbusho ya Taifa(NMT) pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).

Ameeleza kuwa Taasisi hizo zitakuwa na jukumu la kusimamia, kukarabati, kuendeleza, kuendesha  pamoja kutangaza vituo hivyo vyenye utajiri mkubwa wa  kihistoria na kiutamaduni.

 Aidha, kwa mujibu wa tathmini ya ukaguzi iliyofanyika  mwaka jana jumla ya majengo 85 ya kihistoria yalikuwa yapo hatarini kudondoka na kupotea kabisa yasipokarabatiwa.  

Kufuatia hali hiyo Mhe. Kanyasu amesema Taasisi hizo zitasaidia kuyakarabati majengo hayo ili yaweze kurudi katika hali yake ya mwanzo na kuwa kichocheo cha Utalii

Akizungumzia mkakati wa kutangaza vivutio hivyo vya Malikale amesema  vitakuwa vikitangazwa kwa mfumo wa vifurushi (packages) ili kuwawezesha watalii wanapokwenda Mtwara waweze kutembelea vivutio vingi  vilivyopo katika mkoa huo  kwa vile ni ngumu kwa mtalii kwenda Mtwara kwa ajili ya kutembelea mji wa Mikindani pekee.

‘’Tunataka vivutio vya utalii vya Kusini na maeneo mengine ya   nchini yawekwe kwenye vifurushi ili mtalii  akipanga kwa mfano kutembelea mkoa wa Mtwara atembelee Pori la Akiba la Lukwika Lumesule  akitoka hapo atembelee majengo ya kale, ajionee vikundi vya ngoma za asili kisha  aende akapumzike kwenye  fukwe zetu nzuri’’ Amesema.

Awali akizungumza kuhusu majengo ya Kale, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM wa mkoa wa Mtwara, Lukasi Elwesi amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa mikoa ya Kusini imejaliwa kuwa na majengo ya kale mengipamoja na fukwe ambazo hazijaguswa hivyo, ameiomba  Wizara iongeze nguvu katika Kanda hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Malikale, Dkt. Fabian Kigadya amezitaka Halmshauri nchini kulinda na kuendeleza majengo ya kihistoria kwa ajili ya kuvutia watalii hali itakayosaidia kuongeza mapato ya Halmashauri kupitia malikale hizo.
Share To:

Post A Comment: