Mary Sapali, Mratibu Wa Damu Salama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.
Dionisia Simime, Mratibu Wa Damu Salama Halmashauri ya wilaya ya Njombe akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.
  Dkt.Bumi Mwamasage, Mganga mkuu Wa mkoa Wa Njombe akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.
 Mhe. Christopher Ole Sendeka, Mkuu Wa mkoa wa Njombe, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama.

Na. Vero Ignatus.

Kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' imezinduliwa mkoani Njombe, ambapo Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Christopher Ole Sendeka amewataka watendaji kufanya kila wawezalo kuhakikisha kampeni hiyo inaleta tija kwa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga pindi wanapozaliwa.

Kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali kwa wakuu wote wa mikoa nchini katika kuhakikisha vifo vya wajawazito na watoto wachanga vinapungua.

Kampeni hiyo ilizinduliwa Kitaifa mwaka jana mkoani Dodoma na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhudhuriwa na wakuu wote wa mikoa, akiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

Mhe. Ole Sendeka amesema kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' ni ya kitaifa, ikiwa chini ya Raisi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, hivyo watendaji wajipange kuhakikisha malengo yanafikiwa.

"Naagiza Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Njombe, Makatibu Tawala na Wakurugenzi kuhakikisha hatua za kuzuia vifo, ikiwemo kutoa huduma za kitaalamu kwa wakati na kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana katika vituo vya Afya," alisema Ole Sendeka.

Amesema serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha mama wajawazito wanapatiwa ushauri, dawa, kuanzia kliniki hadi pale kujifungua salama

"Mhe Dkt. Magufuli, kwa kuwajali wananchi wake, ametupatia zaidi ya bilioni 3 ili tujenge vituo vya afya katika mkoa wetu, Wakuu wa Wilaya katembelea maeneo ya ujenzi kila mara ili kuhakikisha ujenzi sahihi, kwa matumizi sahihi ya fedha unafanyika," alisema Ole Sendeka. 

Dkt. Bumi Mwamasage ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Bumi amesema uwajibikaji wa kuhakikisha mama wajawazito wanajifungua salama unapaswa kuanzia katika ngazi ya familia.

"Baba na wana familia wanalazimika kuhakikisha mama anahudhuria kliniki ili apate elimu ya ujauzito wake na umuhimu wa chanjo kwa ajili ya kujilinda yeye na mtoto atakayemzaa.

Dkt. Bumi amesema Kampeni hiyo ni ya mwaka mmoja katika mpango wa 'Life Plan' wenye lengo la kuhakikisha hakuna tena vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga, hivyo inabidi jamii yote ishiriki elimu ya kutosha itolewe katika kulikabili tatizo hilo.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliahidi kuchangia shilingi 500,000 Mkuu wa Wilaya 100,000 kila Mkurugenzi, Wenyeviti wa halmashauri Waganga Wakuu wakiahidi kutoa 50,000 ikiwa sehemu ya kuchangia upatikanaji wa Damu Salama wakati wa mama anapojifungua na kutokwa damu nyingi ambao miongoni mwao hupoteza maisha

Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama  inatekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo UNICEF.

Mwisho

Matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.




Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: