Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amesema Sayansi, Teknolojia na ubunifu ina mchango mkubwa  katika ukuaji wa uchumi wa viwanda.

Naibu Waziri Ole Nasha amesema hayo leo wakati wa kufungua mashindsno ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yanayofanyika mkoani Dodoma na kusisitiza kuwa ubunifu na Ugunduzi una fursa ya kuchagiza katika kuongeza tija kwenye viwanda vikubwa, hivyo uhamasishaji wa pamoja unahitajika.

“Hulka ya ubinunifu ni mtu anazaliwa nayo, na kwa jinsi nikivyotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho haya tayari mimi naona wote hapa ni washidi, sasa niishauri Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH - ione  namna ya kuwaendeleza wabunifu wote na usiwe ni kwa wabunifu wachache,”alisema Naibu Waziri Ole Nasha.

Mhe. Ole Nasha amesema kutokana na umuhimu wa wabunifu na wagunduzi nchini ni vyema wananchi wakaendelea kuhamasishwa ikiwa ni pamoja na mashindano hayo yakawa yanafanyija  kila mwaka.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu Profesa James Mdoe amesema lengo la mashindano hayo ni Kukuza hamasa za ubunifu na kuchochea ugunduzi utakao hamasisha Mapinduzi  ya Viwanda.

Baada ya mashindano hayo kutangazwa Wabunifu zaidi 400 walijitokeza kushiriki na kati yao wabunifu 60 walichaguliwa kiushindani  na ndiyo ambao wameshiriki mashindano ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma.

Kauli mbiu ya mashindano hayo ni,  kukuza ujuzi na ubunifu kwa uchumi wa viwanda.

Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
5/3/2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: