Thursday, 28 March 2019

Mtoto wa Ngereza aliza mamia ya watu akisoma wosia alioachiwa na Baba yake


Na. John Walter, Arusha

Mamia ya watu wliohudhuria safari ya mwisho ya kumpumzisha aliekuwa mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One pamoja na mwakilishi wa Idhaa ya Kiswahili (DW) Kanda ya Kaskazini,Charles Ole Ngereza,wamejikuta wakibubujikwa na machozi wakati mtoto wa Marehemu, Faith Ngereza akisoma historia ya marehemu baba yao na wosia aliouacha enzi ya uhai wake.

Katika wosia huo ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza na kusomwa na mtoto wake wa kwanza Faith kwa ujasiri aliwataka watoto wake wasifanye jambo lolote kwa kujionyesha bali wafanye kwa ajili ya kuisaidia jamii kwani wakati wa uhai wake yeye hakufanya kazi kwa kujionyesha kwa watu huku akiwahasa wasikubali kudanganyika na mtu yeyote kwa kuwa dunia ya sasa ukweli haupo ila uongo ili kuufifisha ukweli.

Aidha serikali,Taasisi mbalimbali pamoja na mashirika na jamii za wafugaji wamemlilia Ngereza na kumwelezea kuwa alikuwa ni mwandishi alietizama matatizo ya wananchi waliokuwa wanakosa haki zao haswa wakina mama na jamii ya wafugaji waishio pembezoni mwa hifadhi za wanyamapori.

Nao waandishi wa Habari wakimwelezea Charles Ngereza,wamesema alikuwa ni  mtu asiependa kuona watu wakigombana,alikuwa mpatanishi na anayependa kujifunza na kupokea ushauri.

Mwili wa Charles Ngereza aliefariki akiwa na umri wa Miaka 45 na kuacha mke na watoto wawili na mwili wake umezikiwa nyumbani kwake mtaa wa Baraa jijini Arusha.

No comments:

Post a comment