Baadhi ya wakinamama kutoka kijiji cha kijiji cha Engikaretia wilayani Longido  wanavyoonekana wakiteka maji 

Na. Vero Ignatus, Longido

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uvuvi na mifugo na Maji imetembelea na kukagua mradi ya maji mji mdogo wa Longido ili kuona umefikia hatua gani kimaendeleo

Akisoma ripoti ya maendeleo ya mradi huo Mkurugenzi wa AUWSA Jijini Arusha Mhandisi Ruth Koya amesema kuwa serikali kupitia wizara ya maji na umwagiliaji inatekeleza mradi wa maji safi na salama katika mji mdogo wa Longido ambapo chanzo chake ni mto Simba uliopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro

Amesema mradi huo unategemewa kugarimu kiasi cha shilingi Bilioni 15.8 ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi bilioni 12.3 kimeshalipwa kwa mkandarasi. 

Mhandisi Koya amesema kuwa lengo kuu la mradi ni kuongeza upatikanaji wa maji katika mji mdogo wa Longido kutoka 15%za sasa ambazo ni sawa na wakazi 2, 510 hadi kufikia 100%sawa na wakazi. 16 712 ambapo kiasi hicho kitatosheleza kwa 100% hadi kufikia wakazi 26,145 mwaka 2025

Ameiambia kamati hiyo ya Bunge kuwa mradi huo unauwezo wa kuzalisha kiasi cha lita za ujazo 2,160 kwa siku na mahitaji ya maji ni lita za ujazo 1462 hivyo itaongeza upatikanaji wa huduma ya  maji katika mji mdogo wa Longido wenye jumla ya wakazi 16, 712 kwa sasa, na kufikia wakazi 26, 145 kwa mwaka 2025

Aidha amesema kuwa mradi huo utaondoa magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji safi na salama kwa kijiji cha Engikaretia mbapo utahudumia wakazi wapatao 1294

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati uya kudumu ya bunge ya Uvuvi, Mifugo na Maji  Mahmoud Mgimwa amesema kuwa mradi huo unapokamilika siyo wa serikali bali wenye jukumu la kuutunza na kuulinda ni wananchi wa Longido. 

Amewahakikishia wananchi hao kuwa tayari kamati hiyo imeshazungumza na serikali kuwa ifikapo machi 30 mwaka huu mradi huo utakuwa umeshakamilika na kwamba watarudi tena kwenda kuhakikisha kama kuna mgao wa maji katika maeneo yao. 

'' Leo tumekuja kukagua na kuona tumefikia kwa asilimia ngapi, na mkiona kuna uharibifu wa aina yeyote na nyie mkaa kimya na nyie mtakuwa sehemu ya uharibifu''alisema Katibu huyo
Aidha Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge imemuagiza DC wa Longido pale atakapoona uharibifu wowote kwenye eneo la mradi kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliopo eneo hilo.

 Akizungumza bi Lucy Martini mkazi wa Longido ameiomba kamati hiyo kuhakikisha mradi huo uwe unatoa maji mara zote isijeikawa ni kwa siku moja tu halafu hapo baadae tatizo la. Maji likarudi palepale. 
 Mkurugenzi wa AUWSA jijini Arusha akitoa taarifa ya mradi wa maji mji mdogo wa Longido kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uvuvi, Mifugo na Maji leo wilayani Longido. 
Mkurugenzi wa AUWSA jijini Arusha Mhandisi Ruth Koya akiwa na Katibu wa Kamati ya Bunge ya Uvuvi, Mifugo na Maji 

Mradi wa maji katika kijiji cha Engikaretia kilichopo mji mdogo wa Longido utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 15.8 ambapo hadi sasa tayari makandarasi ameshalipwa shilingi bilioni 12.3 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Uvivu, Mifugo na maji akizungumza na wananchi mji mdogo wa Longido leo,kushoto kwake ni Kaimu katibu mkuu wizara ya maji Emmanuel Kalobelo naibu katibu Mkuu Wizara ya maji  mradi Emmanuel Kalobelo. Picha na Vero Ignatus.
Mkuu wa wilaya ya Longido akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akinamama waliokuja kuteka maji katika kijiji cha Engikaretia mji mdogo wa Longido leo Picha zote na Vero Ignatus 

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: