Friday, 29 March 2019

JK AITAKA TAASISI YA SAYANSI NA BAHARI WILAYANI PANGANI KUENDELEA KUWEKEZA KWENYE UTAFITI

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Sayansi za Bahari kituo cha Utafiti na mafunzo ya ufugaji wa samaki kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah na kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Jaji Damian Lubuva

MKUU wa wilaya ya Pangani Zaibabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mkuu wa Chuo hicho Dkt Jakaya Kikwete
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Damiani Lubuva akizungumza
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Dkt Magreth Kyewalyanga akisoma risala ya chuo hicho
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM akisalimiana na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange mara baada ya kuwasili wilayani humo
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM kushoto akisalimiana na Katibu wa CCM wilaya ya Pangani
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM akisalimiana na Afisa Tarafa wa Pangani mjini Zuhura Rashidi mara baada ya kuwasili wilayani humo
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM  kulia akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Dkt Magreth Kyewalyanga mara baada ya kuwasili chuoni hapo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM  katikati akitembelea maeneo mbalimbali kwenye Taasisi hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Dkt Magreth Kyewalyanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Dkt Magreth Kyewalyanga kulia akisisitiza jambo kwa RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM wakati alipotembelea kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Sehemu ya wakufunzi kutoka Chuo cha Uvuvi Zanzibar wakifuatilia hotuba ya RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM 


RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete ameitaka Taasisi ya Sayansi za Bahari wilayani Pangani Mkoani Tanga iliyopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuhakikisha wanawekeza zaidi kwenye utafiti ili waweze kupata maendeleo makubwa.

Dkt Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Sayansi za Bahari kituo cha Utafiti na mafunzo ya ufugaji wa samaki kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga.

Alisema uwekezaji katika utafiti ndio kichochoe kikubwa ambacho kinaweza kuwapa mafanikio makubwa na hivyo kuwataka kuweka msukumo kwenye suala hilo kwani ndio ambalo linaweza kuwapa mafanikio makubwa

“Nimefurahi sana kwamba taasisi hii ipo kwa ajili ya bahari eneo la viumbe vya majini hakuna taasisi nyengine kubwa kushinda nyie mkibaki kuangalia viumbe vya baharini majini na kusahau na vilivyopo maji baridi kutakuwa na ombwe lakini nafurahi hapa mmeanza kufanya utafiti wa viumbe wa maji baridi”Alisema.

Dkt Kikwete alisema taasisi hiyo imeanzishwa kwa ajili ya ajili ya taaluma kubwa ya viumbe vya bahari huku akiwataka watumie taaluma hiyo kuingiza kwenye viumbe wa maji baridi.

Alisema kwamba taasisi hiyo hiyo ili kuweza kuibua mambo makubwa ya maana ya majini lazima wahakikishe wanawekeza utafiti ambao ndio unaweza kuwafikisha kwenye mafanikio

“Mkitaka kupata maendeleo makubwa lazima muwekeza kwenye utafiti…wakati nilipokuwa Rais niwahi kwenda Korea nikatembela kampuni ya Sumsung na wale wakatupeleka sehemu yao wanaofanyia utafiti wana wafanyakazi zaidi ya 10,000 wakilala wakiamka wana kompyuta mpya na kuwa na vitu vipya walivyo vumbua hivyo lazima tubadilike tufikie huko “Alisema Dkt Kikwete.

Alisema ndio maana Korea ya kusini wamepiga hatua kubwa sana kwa maana wamewekaza kwenye utafiti huku akieleza hata kama wao wakiongeza kitu kingine lakini shabaha yao ibaki kwenye kituo kikubwa cha utafiti.

“Nimelifafanua hili kutokana na maombi yenu mlionipa hapa nimeyapokea nimeyapokea ninayafanyia kazi lakini lazima mtambue kwamba taasisi hiyo shabaha yake kubwa ni kufanya utafiti”Alisema Rais Mstaafu Dkt Kikwete

Alieleza kwamba ziara hiyo ni kuvitembelea baada ya kupewa dhamana ya kuwa Mkuu wa chuo hicho na Rais Dkt John Magufuli hivyo ametembelea ili aweze kufahamu eneo lake la kazi huku akieleza taasisi hiyo ni kwa ajili ya bahari eneo la viumbe vya majini.

Alisema chuo hicho kinafanya kazi kubwa tatu ambazo ni kufundisha, kuzalisha watalaamu wa fani mbalimbali na kufanya utafiti ikiwemo kuhudumia jamii.

Awali akizungumza wakati akisoma risala Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Dkt Magreth Kyewalyanga alisema malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutoa mafunzo ya uvunaji endelevu na uzalishaji wa mazao ya samaki bahari.

Alisema katika tafiti za uzalishaji wa mazao ya bahari taasisi hiyo ilianza na kilimo cha mwani na uzalishaji katika miaka ya 80 ikifuatiwa na tafiti za ufugaji wa smaki aina ya mwatiko ikiwemo uzalishaji wa lulu kwenye miaka ya 2000 na hatimaye utafiti wa perege kuanzia mwaka 2009.

Aidha alisema mazao mengine yanayofanyiwa utafiti na majaribio ni pamoja na majongoo bahari ,kaa koko,chaza,Spirulina nk ambapo tafiti hizo ndio zimechangia sana katika kuwapa ukuaji wa uzalishaji wa viumbe mbalimbali baharini hapa nchini

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alisema uwepo wa chuo hicho ni faraja kubwa sana kwao na kitakuwa kichocheo cha maendeleo kwa wakazi wa wilaya hiyo na kuwashuru chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kukinunua chuo hicho.

Alisem lakini kwa sasa bado changamoto kubwa bado vijana wa Pangani hawajanufaika na chuo hicho ambao wanategemea uwezekaji kwenye sekta ya uvuvi bado hivyo kuomba chuo hicho kuona namna ya kushirikiana na Wizara kutoa mafunzo ya muda mfupi ili ziweze kutolewa kwani faida yake kwa vijana wao wataingia kwenye uvuvi wa kisasa na wananchi watanufaika moja kwa moja.

No comments:

Post a comment