NA HERI SHAABAN

KAMPUNI ya Guru Planet imeandaa mafunzo ya mapishi  kwa vitendo kwa Wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala Aprili 8 mwaka huu.

Mafunzo hayo kwa vitendo yanafanyika Makao makuu ya Kampuni hiyo TABATA Wilaya ya Ilala yatashirikisha Wajasiriamali mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Kampuni ya Guru Planet Nikson Martin alisema mafunzo hayo yatakuwa ya  wiki mbili, dhumuni kuwapa ujuzi wa elimu hiyo Wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala.

"Mafunzo haya kwa vitendo mwaka huu yamelenga kuwafudisha jinsi ya utengenezaji wa kababu, sambusa,bagia, Wali wa maua, pilau, biliani , supu pamoia na keki alisema MARTIN.

MARTIN alisema  wanapokea Wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala pamoja na nje ya Ilala ili uweze kupata fursa hiyo ya Wajasiriamali pekee kwa ajili ya kujiongezea ujuzi.

Aidha alisema washiriki wote watakaoshiriki mafunzo hayo watapewa vyeti vya ushiriki kwa ajili ya kutambulika kuwa amepewa na kampuni hiyo .

 Pia alisema watafundishwa masuala ya afya,mavazi katika sekta ya mapishi, ambapo tunatarajia maafisa afya kutoka wilayani watakuja kuendesha zoezi hilo,  kwa kushirikiana na TFDA .


Mkurugenzi wa Guru Planet aliwataka Wajasiriamali kuchangamkia fursa hiyo   kuwai fomu makao makuu ya kampuni hiyo TABATA.

Alisema dhumuni la mafunzo hayo kuwapa ujuzi katika sekta ya mapishi na kuhakikisha Wanahudumia kwa kuzingatia Afya za Walaji.

Kampuni ya Guru Planet inashughulika kufanya kazi za kuwasaidia Wajasiriamali kupata masoko ya bidhaa zao ,Halmashauri ya Ilala  ilimpatia ridhaa, kibari cha kufanya kazi ndani ya manispaa hiyo .

Aliwataka washiriki kuchukua fomu ya maombi makao makuu ya Kampuni ya Guru Planet TABATA Mtambani  Wilaya ya Ilala.
Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: