Siku ya leo naomba tujifunze elimu mpya kabisa ya uzazi ambapo mwanamke yeyote anaweza kupata ujauzito wenye watoto mapacha hata kama si asili ya ukoo wake, ambavyo wengi wanavyosema.

Nimetumia neno ‘mwanamke yeyote’ kwa sababu kuna imani ya miaka na miaka kwamba, si kila mwanamke anaweza kupata ujauzito bali itategemea na asili yake.

Imani ya kale kuhusu ujauzito
Baadhi ya mila na desturi, hasa katika nchi za Kiafrika zinaamini kwamba, mwanamke kupata watoto mapacha kunatokana na urithi wa kizazi chake, kuanzia mababu wa upande mmoja kati ya wanandoa hivyo uzao huo hufuata mkondo kwa miaka na miaka.

Wengi wakipata mapacha huulizwa kama kwenye kizazi chake, kuna watoto mapacha. Akitokea mama akasema hakuna, basi huaminika kwamba lazima upande wa mwanaume kuna waliowahi kuzaliwa mapacha hata kama si katika miaka ya karibuni.

Imani hii ni ya kizamani sana, ukweli ni kwamba mwanamke yeyote mwenye sifa ya kushika mimba na kuzaa, anaweza kupata ujauzito na kuzaa mapacha bila kujali asili ya kizazi chake.

Kwa nchi zilizoendelea wanawake wanaweza kuzaa mapacha kwa kupandikiza mayai yaliyopevuka kwa kutegemea na idadi unayoitaka mwenyewe lakini bila kujua wangeweza kuzaa hata bila ya kupandikizwa.

Nina ushahidi kuwa, baadhi ya wanawake huenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kupatiwa dawa ya kuwasaidia kuzaa mapacha, jambo ambalo si sahihi na halipo. Sanasana utaliwa pesa zako bure na mapacha usiwapate.

Wanawake wengi wanaoongoza kwa kushika mimba za mapacha ni wale ambao wakati wa kulala wanabadili staili mara kwa mara. Mara nyingi inashauriwa kuwa, mwanamke akishaingia kwenye siku zake za hatari kulingana na mzunguko wake wa hedhi, akutane kimwili na mumewe au mwanaume anayetaka kuzaa naye.

Baada ya tendo la ndoa, mwanaume anashauriwa kulala kwa kujigeuzageuza kitandani. Hapa namaanisha kwamba, akiwa amelala, ajigeuze kuangalia juu, kulalia ubavu wa kulia, kushoto, kulala kifudifudi kwa usiku kucha.

Fanya hivi kwa kurudiarudia siku kadhaa katika kipindi hicho cha hatari, hapo uwezekano wa kushika mimba ya mapacha utakuwa mkubwa sana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: