Thursday, 7 March 2019

DARAJA LA MOMBA KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WANARUKWA

  Daraja la Momba linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Katavi lenye urefu wa mita 84 na kugharimu shilingi bilioni 17.7
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa kapelo) pamoja na wataalamu alioambatana nao wakitembea juu ya daraja hilo ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa daraja hilo lipo tayari kwa matumizi ya kuvuka kutoka mkoa wa Rukwa na kuelekea mkoa wa Songwe.
 Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakitembea juu ya daraja hilo kuonyesha mwanzno wa matumizi ya daraja hilo muda mfupi baada ya kusikiliza nasaha za Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo.
Picha ya pamoja ya wataalamu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa pamojana Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (wa nne toka kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa kapelo)
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewasisitiza wakati wa Kijiji cha Kilyamatundu, Kata ya Kipeta, Wilayani Sumbawanga kuhakikisha wanaitumia vyema fursa inayoletwa kwa kukamilika kwa ujenzi wa daraja la momba ili kuinuka kiuchumi.
Amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo ni kufunguka kwa neema ambayo muda mrefu wanacnhi wamekuwa wakiisubiri na kuongeza kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha inaweka miundombinu sahihi ili kuwarahisishia wananchi wake kupata huduma wanazostahili na sio kuwawekea fedha wananchi mifukoni.
“Kwahiyo daraja hili la mto momba, nina hakika litakuza uchumi wa mikoa yetu, ndani ya mkoa wetu wa Rukwa na mikoa ya jirani, kuna Katavi watakuja kutumia lakini kuna jirani zetu wa Songwe na hata Mbeya, iliyopo ni kuongeza juhudi katika kuzalisha na hasa kilimo cha mpunga ambacho ndicho kinakubali huku, tulime zaidi halafu tuchakate, tuweke viwanda, awali nilishasema na nitarudia tena kutoa wito kwa wadau mbalimbali waje kuweka viwanda huku,” Alisisitiza.
Aidha, alisikitishwa na baadhi ya wafanyabiashra wanaotoka nje ya Mkoa wa Rukwa kuchukua mazao ya mkoa huo na kuyapeleka kwao na kisha kuweka kwenye vifungashio na kudai kuwa mazao hayo yanatoka katika mikoa yao.
Wakati akisoma taarifa ya mradi huo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa Mhandisi Ndelalutse Karoza alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo ni muhimu sana kwa mikoa ya Rukwa na Songwe pamoja na Tanzania kwa ujumla na kubainisha kuwa ukamilifu wa daraja hilo utawainua wananchi kiuchumi na kijamii ikiwemo kupunguza gharama za usafirishaji wa mazao.
“Maendeleo ya kazi hadi kufikia Februari 2019 ni asilimia 95 kwenye daraja na asilimia 97 kwenye barabara za maunganisho, kazi muhimu zimekwisha kamilika na daraja linaweza kutumika, kazi ambazo hazijakamilika ni pamoja na alama za barabarani na kazi ya kuweka taa,” Alimalizia.
Ujenzi wa daraja la mto Momba  linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe kwa upande wa bonde la ziwa Rukwa umefadhiliwa kwa asilimia 100 na serikali ya Tanzania na litagharimu shilingi bilioni 17.7 hadi kukamilika kwake tarehe 24.5.2019 ambapo mpaka sasa limekamilika kwa asilimia 95 na mkandarasi wa ujenzi huo ni Genjio Engineering Group Cooperation kutoka China.

No comments:

Post a Comment