Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa halmashauri ya Temeke wamekutana pamoja na mbunge wao kwaajili ya utambulisho.

Hayo yametokea baada ya mbunge wa halmashauri hiyo Abdalah Mtolea kukihama chama chake cha awali na kuhamia CCM mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalah Mtolea amesema muda wote walikuwa hawajatambuana kutokana na kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo na kutofanya kampeni.

“Jimbo la Temeke ni moja kati ya halmashauri zilizofanikiwa kupata udhamini wa kutengeneza miundombinu huku halmashauri kupata zaidi ya bilioni 265 kwa ajili ya kukarabati miundombinu”. Amesema Mtolea.

Aidha Mtolea amesema Jimbo la Temeke si lile ambalo lilikuwa zamani kutokana na miundombinu kutengenezwa katika kata mbalimbali za halmashauri za Temeke.

“Ukipita katika kata ya Kilakala zamani kulikuwa na madimbwi matupu haikuwa na barabara hata moja ya lami, Leo hii kuna barabara za lami zaidi ya tisa zimejengwa  na nyingine zimeunganisha kata nyingine”. Ameongeza Mtolea.

Kwa upande wa Katibu wa UWT kata ya Kurasini Mwamvita Mbaruku amesema amefurahi kupata fursa kuja kuonana na kutambulishana na Mbunge wao ambaye kwasasa yupo CCM.

“Mtolea ameona katika upande wa pili kasi yake ilikuwa ndogo na ndo maana akaamua kumuunga mkono muheshimiwa rais Magufuri”. Amesema Mwamvita.
Share To:

Post A Comment: