Katibu wa CCM Mkoa Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Steven Kebwe
 Meza kuu
 Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho


Na Mwandishi wetu Morogoro

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Ndugu Innocent Kalogeris Leo Amefungua Kikao cha Kazi Cha Madiwani wa CCM wa Kata 143 za Halmashauri Tano za Mkoa wa Morogoro ambazo ni Gairo, Kilosa, Mvomero, Morogoro Mjini na Morogoro Vijijini.

Kikao Hiki Kimeudhuriwa na Mameya wa Halmashauri ambao wanatokana na Chama Cha Mapinduzi, Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Stephen Kebwe, Katibu wa CCM Mkoa Ndugu Shaka Hamdu Shaka,na Wenyeviti na Makatibu wa Wilaya zote Tano.

Katika Kikao Hiki Madiwani walipata Nafasi ya Kutoa Changamoto na Kero Mbalimbali zinazowakumba Wananchi Wanaowaongoza na Namna Gani ya Kutatuliwa ili kuwaondolea Wananchi Mzigo na Kutimiza Maagizo ya Katibu Mkuu CCM Taifa Dr Bashiru Ally ya Chama Kushughulika na Shida Za watu.


Katika Kikao Hicho, Madiwani Wameeleza Changamoto za Ukosefu wa Maji, Umeme, Barabara Hasa zilizochini ya TARURA, Migogoro Ya Wakulima na Wafanyakazi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Steven Kebwe alipata Nafasi ya Kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020 na Pia Kujibu Hoja zilizoibuliwa na Madiwani Hao ikiwepo baadhi ya Wananchi kuwekwa ndani na wakuu wa Wilaya na amepiga Marufuku wakuu wa Wilaya Wote Mkoa wa Morogoro kuwaweka ndani Raia Bila Sababu za Msingi na Pia Amehaidi Changamoto zote Zilizoibuliwa na Madiwani Hao Kushughulikiwa kwa Haraka.

Aidha Katika Kikao Hicho Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Ndugu Shaka Hamdu Shaka Amemshukuru Rais Dr John Pombe Magufuli Kwa Juhudi zake za Kuhakikisha Fedha za Kutosha Zinapatikana Katika Sekta ya Afya, Elimu Bure, Miundombinu, Maji Safi na Salama, Umeme Vijijini na Utatuzi wa Migogoro ya Wakulima na Wafanyakazi ambayo Imepungua kwa Kiasi Kikubwa Tangu Serikali ya Awamu ya tano Chini ya Rais Magufuli iingie Madarakani.

Katibu Shaka Amemaliza Kwa Kuwaomba Madiwani na Viongozi wa Chama wa Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Kuendelea kushirikiana Pamoja na Kutokukubali Kugawanyika Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020.
Share To:

Post A Comment: