Watendaji hao wapo nchini kwa ziara ya kawaida ya kikazi ya siku tano ambapo waliomba kukutana na Waziri wa Madini.

Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo inakusudia kuwasilisha taarifa juu ya hali na Maendeleo ya soko la dunia kwa Madini ya Rare Earth Elements na kuzungumzia hatua iliyofikiwa kwa ombi la leseni ya  uchimbaji  Mkubwa wa madini hayo.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko  amesema wizara iko tayari kuipokea kampuni husika nchini baada ya kukamilika kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu Rocky Smith, amesema kuwa, amefurahishwa na  ushirikiano unaooneshwa na wizara na kuahidi kuanza shughuli za uchimbaji mara baada ya kukamilika kwa taratibu
Share To:

msumbanews

Post A Comment: