Na John Walter-Babati

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr. Faustine Ndugulile amemwagiza Mganga Mfawidhi wa  Kituo Cha Afya Magugu Dkt. Eriara Palangyo kurudisha fedha kiasi cha TSh. 30,000 za dawa kwa mgonjwa baada ya kutozwa fedha za matibabu wakati kuna dawa za kutosha kituoni hapo.

Dkt. Ndugulile ametoa  agizo hilo baada ya kubaini mgonjwa aliandikiwa kununua dawa nje ya kutuo wakati dawa hizo zikipatikana kituoni hapo baada ya kufanya mahojiano na baadhi ya wagonjwa hospitalini  hapo.

Mgonjwa huyo ambaye hakutaaka kutaja jina lake alimwambia Naibu Waziri Dkt. Ndugulile kuwa alinunua dawa hizo kwa thamani ya shilingi 30,000 lakini wakati dawa hizo kama angezinunua kutoka dirisha la dawa la serikali hospitalini hapo ghalama yake ingekuwa shilingi elfu mbili.
 Naibu Waziri huyo baada ya kukagua boari ya dawa kituoni hapo alibaini uwepo dawa za kutosha na  dawa alizoandikiwa mgonjwa huyo zikiwepo hospitalini hapo lakini pia aligundua kuwa wataalamu wa dawa hawakuwa wakifanya kazi kwa waledi kitaaluma kwani walifanya kazi bila kutoa orodha ya dawa iliyopo kumwezesha Daktari kumwandikia dawa mgonjwa kwa orodha ya dawa iliyopo.

Akiongea na wafanyakazi baada ya  kumaliza ukaguzi wa kituo hicho cha Afya Naibu Waziri Ndugulile katika majumuisho yake alisema kimsingi hajaridhishwa na utendaji kazi wa kituo hicho kwa kuwa uwekaji kumbukumbu kituoni hapo haukuwa vizuri.

Pamoja na makosa katika kuweka kumbukumbu za matumizi ya dawa lakini pia kituo hicho kimeshindwa kutoa huduma kwa kuzingatia mpango wa Wizara wa uhakiki ubora kwa kuwa mpaka sasa  bado Kituo hajakipanda hadhi ya kuwa kati ya vituo vyenye nyota zaidi ya moja.
Akiwa kituoni hapo pia alitoa elimu ya kutambua dawa za serikali zenye nembo ya MSD kwa kamati ya ulinzi na usalama akitaka kamati hiyo kutambua kuwa kukuta mtu anauza  dawa zenye nembo ya MSD ni sawa na kumkuta mtu na pembe za ndovu.

Kufatia hali ilivyo kituoni hapo Dkt. Ndugulile alimpa Mkuu huyo miezi miwili kufanya marekebisho katika kituo hicho vinginevyo alishafikilia kumtoa lakini akachagua kumsamehe na kumpa zaidi muda wa kujirekebisha.

Naibu Waziri  Ndugulile alifanya ziara ya ghafula kituoni hapo mara baada ya kuwa ametembelea pia makao ya wazee wasiojiweza magugu ikiwa ni mojawapo ya shughuli zake mkoani Manyara ambapo yuko mkoani humo kwa ziara ya siku tatu kujionea baadhi shuguli zinazosimamiwa na Wizara yake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: