Saturday, 3 November 2018

Dc Muro Akabidhiwa Mifuko 75 ya Saruji na Mil. 5 kwa ajili ya ujenzi wa Vyoo vya Shule ya Seliani


 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro Akikabidhiwa mifuko ya Saruji kutoka kwa mdau wa maendeleo Ndg. Ramadhani Nangu mwakilishi wa Bwana Manglan anayeishi nchini Marekani kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule ya Seliani kilicho titia wiki iliyopita.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro,sambamba na  Katibu Tawala wa Arumeru Mwl. James Michembe pamoja na Mkurugenzi Halmashauri ya Arusha  wakipokea msaada wa Fedha Tsh. Milioni Tano kutoka kwa Ndg. Joel Nathaniel Sasali ambaye ni Operesheni Meneja wa Kampuni ya Usafirishaji ya Dar Lux akiwa ameambatana na baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Akipokea Vyoo Ishirini kutoka kwa Mdau wa maendeleo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo cha wananfuzni wa shule ya msingi Seliani kilichotitia .
 Mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi akikabidhi mchango wa ujenzi wa choo kilichotitia kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro.

Na, Imma Msumba Arumeru

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro Amepokea misaada ya saruji mifuko 75,   shilingi milioni 5 pamoja na vyoo 20 vya kisasa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Seliani kilichotitia wiki iliyopita.

Akizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo Dc Muro amesema kuwa misaada hiyo itasaidia kufanikisha ujenzi wa vyoo hivyo kwa muda mfupi, Pia amewashukuru sana wadau wa kampuni ya Usafiri ya Dar Lux kwa msaada wa Milioni Tano ( 5 ).

kwa upande wake Ndg. Nangu amesema wamejitolea Saruji hiyo kwa ajili ya vyoo vya kisasa kabisa  yenye thamani ya sh.milioni Moja na Laki moja na ishirini na tano kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Dc Muro baada ya kupata Taarifa za janga la kutitia kwa choo hicho.

  “Tunatambua changamoto wanazopata wanafunzi hasa kwa mtoto wa kike kutokana na maumbile yake, hivyo ujenzi wa vyoo hivi  utasaidia kuwafanya wanafunzi hao kufurahia mazingira yatakayokuwamo wakiwa shuleni,” alisema Nangu.
Alisema wanafahamu matatizo wanayoyapata watoto wa kike wakiwa shuleni hasa wanapofkia hatua ya kuvunja ungo, kutokana na mabadiliko yanayoanza kutokea na wanapokuwa kwenye tarehe zao ambapo wengine hulazimika kutokwenda shule kutokana na mabadiliko yao ya kimwili, hivyo  kwa kushirikiana na Dc Muro wanaamini ujenzi wa vyoo hivyo utawaondolea mabinti wasiwasi.

No comments:

Post a comment