Tuesday, 30 October 2018

Lady Jaydee, Prof. Jay na Afande Sele watajwa na Izzo Bizness kwenye hili

Msanii wa muziki hip hop Bongo, Izzo Bizness amewataja wasanii watatu wa wa Bongo Fleva ambao anatamani kufanya nao kazi.

Rapper huyo kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM amewataja wasanii hao kuwa ni Lady Jaydee, Prof. Jay  na Afande Sele.

"Natamani kufanya na Dada yetu Lady Jaydee, wengine kwa haraka haraka ni  Afande Sele na Professor Jay," amesema Izzo.

Kwa sasa Izzo Bizness anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Nimedata ambao amemshirikisha Jay Melody.

No comments:

Post a comment