Mbunge%2Bwa%2Bjimbo%2Bla%2Bchalinze%2BRidhiwani%2BKikwete%2B%2Bakisisitiza%2Bjambo%2Bkwa%2Bwanafunzi%2Bwa%2Bshule%2Bya%2Bsekondari%2Bchalinze%2Bambapo%2Baliwataka%2Bwanafunzi%2Bhao%2Bkuacha%2Bkukaa%2Bvijiweni%2Bmara%2Bbaada%2Bya%2Bmasomo%2Byao.Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chalinze katika mahafari ya shule hiyo.Ridhiwani%2BKikwete%2Bmbunge%2Bwa%2Bchalinze%2Bakimkabidhi%2Bmmoja%2Bwa%2Bwanafunzi%2Bwa%2Bshule%2Bya%2Bsekondari%2Bcheti%2Bcha%2Bufaulu%2Bbora%2Bwa%2Bsomo%2Bla%2Bkiswahili.
Wanafunzi%2Bwa%2Bshule%2Bya%2Bsekondari%2Bchalinze%2Bwakiwa%2Bna%2Bnyuso%2Bza%2Bfuraha%2Bhuku%2Bwakimsikiliza%2Bmgeni%2Brasmi%2Bkatika%2Bmahafari%2Byao.
Baadhi ya wananfunzi.


Na Shushu Joel,Chalinze

VIJANA wengi nchini wamejikuta wakikumbana na changamoto nyingi katika utafutaji wa maisha katika jamii zao na kupelekea kundi jingine kujiunga katika matumizi hatari ya utumiaji wa madawa ya kulevya na hivyo hata taifa kukosa vijana wa kuitumikia serikali yao.

Kukithili kwa vitendo vya uvutaji wa bangi vijiweni kunasababishwa na wazazi walio wengi kwa kutojenga tabia ya kuwakanya watoto wao pindi wanapokuwa wadogo na hata inapotokea watoto wao kupewa hadhabu ya viboko na walimu au watu wengine wazazi wamekuwa wakiwaijua juu wale waliojitokeza kuwakanya watoto hao.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chalinze katika mahafari ya shule hiyo mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amewataka vijana kutokaa vijiweni na watu walioshindikana kwani watawashawishi vibaya na hata kuwataka waweze kujiunga katika makundi ambayo si mazuri.

Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakishawishiwa na watu wenye nia mbaya na vijana ili kuwaona tu na wao wanaharibika kwa kufuata matendo mabaya wanayoyafanya kwenye mitaa ikiwemo ubakaji,uvutaji wa madawa ya kulevya na hata kwenye wizi.

Kikwete aliongeza kuwa serikali inawategemea kwa kiasi kikubwa ili muweze kuja kuisaidia katika Nyanja mbalimbali pindi mtakapokuwa wakubwa kwani uongozi ni mchezo wa kupokezana.

“Mimi mbunge wenu nawahakikishieni serikali ya awamu ya tano imekuwa imejiwekea mikakati mikubwa ya kuhakikisha vijana wote wanamaliza masomo yao na wanafaulu ni lazima waende shule bila cha kusingizia kukosekana kwa ada,hivyo nawatakeni wanafunzi wote katika jimbo la chalinze kuhakikisha kila mmoja wenu anafaulu ili kuja baadae kuisaidia serikali na Taifa kwa ujumla.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imrvutakila aina ya michango mashuleni kwa madhumuni ya kuona watoto wanapata elimu ya kutosha pia kuongeza ufaulu kwa watoto” Alisema Kikwete.

Shaabani Husein ni mmoja wa wahitimu katika shule hiyo alisema kuwa anampongeza mbunge wa jimbo hilo kwa mchango mkubwa anaoufanya kwa vijana wa shule hiyo kwa lengo la kuhakikisha vijana wanasoma kwa bidii bila matatizo ya aina yeyote ile.

Aliongeza kuwa ushauri uliotolewa ni mkubwa sana hivyo tunamuhakikishia mbunge kuwa hakuna kijana atakaye potea katika na kujiingiza katika mambo maovu ya uvutaji wa bangi,wizi na utumiaji wa madawa ya kulevya kutokana na wengi wetu kutambua madhara yake.

Aidha alisema kuwa wazazi walio wengi wamekuwa wakichangia watoto kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya kutokana na kutokutumia muda wao wa ziada kutuelimisha majumbani kwetu na badala yake kazi kubwa kuwaachia walimu tu.

Naye Mriamu Patrik alisema kuwa madawa ya kulevya yanachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza nguvu kazi ya vijana wetu ambao mara baada ya kujidunga madawa hayo ulala tu hivyo kupelekea watu hao kutokuwa na nguvu za kufanya kwani miili yao uzoefu.

“Nampongeza mbunge Ridhiwani Kikwete kwa ushauri alioutoa kwa vijana juu ya kutambua jinsi gani ijana na kumhakikishia kuwa vijana hao wa shule hiyo wanazingatia kila ushuri wa viongozi wao wa dini na wale wa serikali kwani wanahitaji tuwe kwenye maisha yanayositahili”Alisema

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Emanuel Kahabi amewapongeza wanafunzi wake wanaotarahiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu kwa nidhamu kubwa wanayoionyesha shuleni na mitaani hii ni kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya walimu na wazazi katika kuwajengea watoto hao maisha yao ya baadae.

Aliongeza kuwa wanafunzi watakao maliza kidato cha nne mwaka ni 307 hivyo kulingana na vile walivyowaandaa wanatarajia matokeo mazuri yatakayofurahisha zaidi ya mwaka jana.

Aidha amempongeza mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete kwa misaada mbalimbali anayoitoa katika shule hiyo kwa lengo la kuhakikisha shule hiyo inakuwa miongoni mwa shule za kisasa na za kuvutia katika jimbo lake.

“Mbunge wetu katusaidia vitu vingi katika kuhakikisha shule hii inakuwa ya kipekee kwani katuwesheza komputa,mabati,saruji,mbao na vitu vingine vingi nab ado anaendelea kutusaidia kweli huyu ni kiongozi wa kipekee sana” Alisema mkuu wa shule hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: