Rais John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi,Kamanda wa polisi wa wilaya ya Kyerwa Justine Joseph na Mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Kyerwa Everist Kivuyo na Mkuu wa kituo cha polisi Kyerwa Robert Marwa.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu,Viongozi hao wa polisi wanasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhusika katika magendo ya zao la kahawa katika wilaya ya Kyerwa pamoja na tuhuma nyingine zilizobainika wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani humo.
Share To:

Anonymous

Post A Comment: