Monday, 10 September 2018

Wafugaji kutokomeza mila zinazokiuka haki za binadamu


Na Ferdinand Shayo,Manyara.

Viongozi wa mila wa jamii za kifugaji kutoka kijiji cha Namalulu ,kata ya Naberera ,Wilaya ya Simanjiro  wamesema kuwa tayari wameanza kutokomeza mila zinazokiuka haki za binadamu ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni ili kuhakikisha ustawi bora wa jamii utakaochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Aidha Kiongozi huyo Meshack Torero amesema kuwa watashirikiana na viongozi wa serikali kuhakikisha kuwa wanatokomeza mila hizo ambazo zimekua zikiwanyima watoto wa kike fursa ya kupata elimu na kujikuta wakitumbukia katika mimba za utotoni na kuolewa katika umri mdogo.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula wamesema kuwa hali ya ukeketaji imepungua kwa kiasi kikubwa ili kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali,viongozi wa mila pamoja na asasi za kiraia katika kuhakikisha kuwa suala LA ukeketaji linatokomezwa ili kuondoa mila kandamizi zinazokiuka haki za binadamu.

Kwa upande wao Wakazi wa Kijiji hicho Joyce Laizer wamesema kuwa viongozi wa mila na serikali inapaswa kukemea suala la ndoa za utotoni pamoja na utumikishwaji wa watoto wanaochunga mifugo na kukosa haki ya kupata elimu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: