Wenyeviti 20 wa vijiji wa Chadema katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro wamehamia CCM leo Alhamisi Septemba 6, 2018.

Mbunge wa Hai ni Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi za Upinzani Bungeni.

Majina ya wenyeviti hao na vijiji vyao katika mabano ni, Hendry Kimaro (Lukani), Josephat Joseph (Mbosho), Comred Munuo (Kyuu), Elibariki Mbise (Rundugai), Nassor Mushi (Wari Sinde), Erasto Mushi (Kyeeri), Iddy Mtambo (Chemka), Seth Munisi (Uraa), Issa Kisanga (Kware) na Paradiso Munisi (Uswaa).

Wengine ni  Emanuel Mbowe (Nshara), Simbo Mbasha (Mungushi), Bethuel Swai (Isawerwa), Godfrey Kivuyo (Jiweni), Joel Kalungwana (Nerere), Emanuel Laizer (Mlima Shabaha), Michael Kiwelu (Kambi ya Raha), Godfrey Maimu (Umoja), Witness Mwanga (Sonu).

Mkurugenzi wa halmshauri ya Hai, Yohana Sintoe amethibitisha kupokea barua za kujiuzulu za wenyeviti hao.

Amesema kulikuwa na wenyeviti 19 lakini baadae akaongezeka mmoja na kufikia 20. Hata hivyo mwenyekiti huyo wa  20 jina lake halijapatikana.

Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema anawapongeza viongozi hao kwa kutumia haki yao kidemokrasia na kujiuzulu.

Sabaya amesema kwa sasa hakuna Mtanzania ambaye haoni kazi nzuri za Rais John Magufuli hivyo viongozi hao kujiuzulu wameonesha heshima kwa Rais.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: