Diwani wa kata ya Majengo katika Halmashauri ya Meru kupitia (Chadema), Ndg. Bernard Wilson Kivondo ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM kwa maelezo kwamba amefurahishwa na utendaji kazi na anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Kivondo ni diwani wa kumi katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kipindi hiki na kujiunga na Ccm  kwa  kumuunga mkono Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Emmanuel Mkongo amethibitisha leo ( 03 September 2018 ) kupata taarifa za kujiuzulu kwa Kivondo.





Share To:

msumbanews

Post A Comment: