Wednesday, 5 September 2018

DC KIMANTA APOKEA VIFAA TIBA VYA THAMANI YA MILIONI KUMI NA TISA


Mkuu wa wilaya ya Monduli mh.Idd Hassan Kimanta pamoja na mganga mkuu wa wilaya ya monduli Titus Mmasi walishiriki kupokea Vifaa tiba vilivyo tolewa na shirika la Pathfinder.

Mkuu wa wa wilaya alipokea vifaa hivyo akiwa kituo cha afya cha Mto wa mbu amevipokea kutoka kwa Meneja wa mradi Bw.Anjelo kihaga.Mkuu wa wilaya amepokea kitanda cha upasuaji (OPERATING BED) chenye thamani ya milioni 19.

Shirika hilo hilo la Parthfinder la kimataifa lililo sajiliwa hapa nchini Tanzania linalofadhiliwa na shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID)inatekeleza miradi mbalimbali kwa miaka mitano shirika hilo linafanya kazi katika hifadhi za Taifa (TARANGIRE NATIONAL PARK ECOSYSTEM) Kwa lengo la mradi wa watu,afya,mazingira,uzazi wa mpango,cocoba na boma za mfano.

Mkuu wa wilaya amelishukuru shirika hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa shughuli za maendeleo wilayani monduli
 nakuahidi kuvisimamia na kuvitunza vifaa hivyo walivyo pewa.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: