Na. Vero Ignatus  Ngorongoro

OXFAM kwa kushirikiana na Shirika la PALISEP wameendesha mafunzo ya teknolojia ya kidigitali kwa wananchi wilaya ya  Ngorongoro mkoani Arusha ili kuleta  maendeleo katika jamii husika. 

Maratibu wa Teknolojia kwa maendeleo shirika la Oxfam Bill Marwa amesema  wametoa mafunzo kwa wananchi zaidi ya (90)yakiwa na lengo la wao kutambua namna ya kuitumia mitandao hiyo pamoja  nyenzo mbalimbali za kidigital kwa kutuma ujumbe mfupi, kutoa taarifa kwa viongozi wao wa kijiji,kujibuwa changamoto wanazokutana nazo kwaajili ya kujiletea maendeleo.

 "Kadri miaka inavyoenda kumekuwa na ongezeko la mitandao ya kijamii ulimwenguni hivyo Oxfam kama shirika limeona upo umuhimu wa maendeleo, kupata taarifa, kutoa matokeo"alisema Bill Marwa.Washiriki wa mafunzo hayo walifundishwa sheria za mtandao 2015 pamoja na makosa ya mtandaoni, jinsi ya kutumia vifaa hivyo katika namna ambayo havivunji sheria ya nchi. 

Sambamba na hayo walifundishwa maswala Mbalimbali jinsi ya ukingi haswa kwa wanawake kulinda haki za mwanamke na kupinga ukatili wa kijinsia dhidi yao.Mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku nne yaliyoshirikisha kata zaidi ya 10 katika wilaya ya Ngorongoro,ikiwa ni mradi wa  miaka miwili unaotekelezwa katika mikoa (4) Arusha, Geita,Kigoma,na Mtwara katika wilaya za Mtwara vijijini, Mbogwe Geita, Kibondo,na Ngorongoro. 

Mradi huo unalengo la kuwawezesha wananchi kutumia nyenzo za digitali ili kujiletea maendeleo katika jamii husika,amabapo ulianzishwa rasmi mwaka 2016 desemba na unatarajiwa kumalizika novemba 2018 ,mradi huo upo chini ya ufadhili kutoka nchini Ubelijiji. 
 Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini kile kinachofundishwa kuhusiana na matumizi ya digitali sambamba na mitandao ya kijamii
Meneja wa Program Shirika la Oxfam Kefar Mbogela akitoa Elimu namna ya kutumia mitandao na nyenzo mbalimbali za kidigitali bila kuleta madhara kwa jamii wala kuvunja sheria ya mitandao hiyo
Rachel yeye anasema mwanzoni alikuwa akitumia simu ya hali ya chini ambayo alikuwa hapati mambo mengi ya faida ,ila kwa sasa mara baada ya kupewa simu na Oxfam imemsaidia sana kuweza kuwasiliana na na jamii ,amesema kwasasa anaweza kupaza sauti kwa kutumia simu yake,kutatua changamoto mbalimbali na viongozi wanapoona ujumbe wake wanatatua tatizo na majibu yanapatikana kwa wakati.
Darasa la mafunzo ya kutumia nyenzo za mitandao ya kijamii na namna ya kutumia nyenzo za kidigitali yakiendelea.
Ndugu Ezekiel Ndukumat kutoka Kijiji cha Pinyinyi tarafa ya Sale wilaya ya Ngorongoro amesema yeye anapata habari za kila sehemu kwa muda wowote ,pia jamii yake imenufaika kupitia , uragabishi wa kutumia njia ya digitali,ujumbe unakwenda kwa haraka na wanapata majibu kwa wakati.
Norkitoi Lengela kutoka kijiji cha Piyaya kata ya Piyaya wilaya ya Ngorongoroanasema amepata faida kubwa sana kupata simu kwani ameelewa jinsi dunia inavyokwenda tofautina awali,pia amefahamu kuwa ipo faida ya kuisaidia jamii yake,pia ukaribu wake na viongozi wa kijiji,amesema tukio likitokea kijijini kwake anaitwa na kuambiwa alirushe ili waweze kupata msaada wa haraka.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya KONCEPT inajihuisha na masuala la ya ushauri wa masoko,matangazo,mahusiano kwa umma na mitandao yakijamii  Krantz Mwantepele akitoa elimu lwa wananchi wa Ngorongoro namna ya kutumia simu zao kwa faida .

Mafunzo yakiendele namna ya kutumia Digitali kwa kuleta maendeleo katika jamii husika na kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo.
Wananchi wakifuatilia kwa makini kile kinachofundishwa kuusiana na matummizi ya mitandao ya kijamii na nyenzo mbalimbali za kidigitali
Wananchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo namna ya kutumia mitandao ya kijamii na nyenzo za kidigitali Loliondo(w)Ngorongoro  mkoani Arusha.
Wananchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo namna ya kutumia mitandao ya kijamii na nyenzo za kidigitali katika Hotel ya Flamingo Safari iliyopo (w)Karatu mkoani Arusha. Habari / Picha :VERO IGNATUS 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: