Saturday, 4 August 2018

Zaidi ya Wanachama 400 wa Chadema wilayani Arumeru wajiunga na Ccm


Zaidi ya wanachama 400 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wengi wao wakiwa vijana wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM katika Kata ya Songoro Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha.

Maamuzi ya wanachama hao yametokana na kampeni za kunadi sera ya CCM zinazoendelea katika kata  hiyo ya Songoro ambazo zinafanywa na mgombea wa Udiwani Ndg. Charles Nnko.


Mmoja kati ya vijana ambao wamekihama Chama cha CHADEMA na kujiunga na CCM, akielezea  sababu za kukihama chama hicho katika mkutano wa kampeni ambao.

Amesema kuwa 

"Sababu ya kwanza ni vyama vya upinzani ikiwamo Chadema kushindwa kujipambanua kama taasisi, badala yake kuwa kama cha mtu binafsi,pia ni ukosefu wa maamuzi shirikishi, ukiukwaji wa katiba na misingi ya demokrasia, kutokuwa na mawasiliano na umoja na kukosa maadili kwa viongozi."

Wanachama Hao wapya wamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro, Mbunge wa Longido Dr. Kiriswa Pamoja na Uongozi wa Chama Wilaya ukiongozwa na Katibu wa Ccm Wilaya.

Matukio Mbalimbali katika picha.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: