Saturday, 11 August 2018

WAZIRI WA MADINI ANGELA KAIRUKI AWAPA ONYO WATOROSHAJI WA MADINI YA RUBY MUNDARARA LONGIDO


Mkuu wa wilaya ya Londigo Frank Mwaisumbe akiuelekeza msadara wa Waziri wa Madini Angela Kairuki aliyefanya ziara kwenye mgodi wa Mundarara Ruby Miningi unaomilikiwa na mwekezaji Rahim Mollel uliopo Kata ya Mundarara katika ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. 
Waziri wa Madini Angela Kairuki akiangalia kwa makini mgodi wa madini ya Ruby wa Mundarara unaomilikiwa na mwekezaji Rahimu Mollel ambapo alifanya ziara hiyo kujionea shughuli za uchimbaji na kufahamu changamoto zinazowakabili.
Mwekezaji wa mgodi wa Mundarara Ruby Mining uliopo Longodi mkoani Arusha Rahim Mollel akiongoza msafara wa Waziri wa Madini Angela Kairuki aliyefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutembelea mgodi huo. 
Mwekezaji wa mgodi wa Mundarara Ruby Mining uliopo Longodi mkoani Arusha Rahim Mollel akimuonyesha Waziri wa Madini kipande cha Ruby mara baada ya kuvunja jiwe gumu. 
Waziri wa Madini Angela Kairuki akisoma Leseni ya uchimbaji ya kampuni ya Sendeu inayomilikiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Mbunge wa zamani Longido Michael Laizer 
Waziri wa Madini Angela Kairuki akiangalia mazingira ya mgodi wa uchimbaji madini ya vito ya Ruby unaomilikiwa na Kampuni ya Sendeu iliuopo chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Mbunge wa zamani Longido Michael Laizer.
Waziri wa Madini Angela Kairuki akicheza ngoma za kabila la Wamaasai kabla ya kuwahutubia wananchi na wakazi wa Kijiji cha Mundarara yalipo machimbo ya madini ya vito ya Ruby wilayani Longido mkoani Arusha. 
Waziri wa Madini Angela Kairuki akihutubia wananchi na wachimbaji wadogo wa madini ya vito ya Ruby katika eneo la Kijiji cha Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha.


WAZIRI wa Madini Angela Kairuki amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya Vito ya Ruby katika Kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha kujitafakari upya na kuwa wakweli katika biashara hiyo ya madini. 

Akiwa katika ziara yake ya kikazi iliyolenga kujionea shughuli za uchimbaji wa madini hayo ya vito pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili Waziri Kairuki alifanya pia mkutano mkubwa wa hadhara kijijini hapo. Akizungumza na wananchi hao wa Mundarara Waziri Kairuki aliwataka wananchi hao kushirikiana na Serikali katika kuwafichua watu wasiowaaminifu kwa rasilimali za taifa. 

“Nyinyi wananchi na wafanyabiashara hapa mnawajua wanaotorosha madini kwenda nchi jirani, niwaombe muwafichue kwani madini hayo ni fedha mnazozihamishia nchi nyingine ambazo zingewaletea maendeleo nyinyi. “Tafadhaili sana kwa wafanyabiashara naowamba muache kuanzia sasa kwani mtajikuta mkiwa katika wakati mgumu wa kupteza mitaji yenu na hata kupoata hasara kubwa pindi mtakapokamatwa,” alisema Waziri Angela. “Kiama kikubwa kinakuja kwa watoroshaji wote wa madini sasa nimekuja hapa kuwaambia ole wao wanaowasaidia na wanaoshirikiana nao haoa mpo karibu na mpaka nawaomba mjiepushe na biashara hiyo haramu,” alisema. 

Kupitia ziara hiyo Waziri Kairuki alitumia fursa hiyo kuwataka wawekezaji kumaliza migogoro ya mitobozano inayowakabili ambapo pia alifanya ziara katika Mpaka wa Namanga kwa lengo la kujionea changamoto zinaawakabili wafanyakazi wa wizara hiyo. 

No comments:

Post a comment