Tuesday, 28 August 2018

Vijiji vyote vya Iramba kufungwa umeme wa REA


MENEJA wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kanda ya Kati, Mhandisi Athanasio Nangali amesema watahakikisha vijiji vyote vya Wilaya ya Iramba ambavyo havijapata umeme wa REA mzunguko wa tatu kwa awamu ya kwanza, na awamu ya pili, vinapatiwa umeme huo.

Akizungumza jana katika Kata ya Ndurungu wilayani Iramba mkoani Singida, Eng Nangali alisema watahakikisha kuwa ifikapo mwaka 2021 umeme unaenea katika mkoa wote wa Singida kwa takribani vijiji 150 vilivyoko kwenye mpngo

Alisema kuwa Wilaya ya  Iramba ina vijiji 30 ambavyo vinatakiwa kuwekewa umeme wa REA na kwamba kuna baadhi ya vijiji ambavyo viliachwa kwenye awamu hiyo.
jb
"Kwa kuwa mbunge wenu amekuja kuomba vijiji vya Kata ya Ndurungu ikiwemo Kipuna , Mahola na Mwanduigembe viweze kupatiwa umeme katika awamu hii. Tutasimamia kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme kwani ndio chachu ya maendeleo  na ndio fursa nyingi zitapatikana," alisema Eng Nangali.

Kwa upande wake, Mbunge wa Iramba, Dk Mwigulu Nchemba alisema amepeleka maombi hayo kwa sababu baadhi ya vijiji havijapata umeme kwa muda mrefu licha ya kuzungukwa na maeneo mengine yenye umeme.

Dk Nchemba alisema Kata ya Ndurungu imezaliwa kutoka Kata ya Kaselya ambayo ina umeme hivyo wanakijiji wake wanaona kama wametengwa.

"Wanakijiji hawa wanaona wametengwa ili wakose huduma hiyo muhimu au wametengwa ili wapate huduma. Niliona nipeleke maombi maalum ili Kata hii ipate umeme," alisema Dk Mwigulu.

Pia alisema Kijiji cha Sipuka tayari kina umeme na kwenye mpango huo unataka uende kijiji cha Mnere kuzunguka Kata hiyo.

Alisisitiza kuwa kijiografia wananhi wote wanahitaji huduma ya umeme kwani zipo shughuli nyingi za maendeleo zinazofanyika ikiwemo hospitali, shule na viwanda.

Naye, Mwanakijiji wa Mwandujembe Kata ya Ndurungu, Omary Hussein alisema ujio wa umeme utasaidia wajasiriamali, viwanda na shughuli nyingine za maendeleo.

Alisema suala la umeme lilikuwa ni ndoto yao ya muda mrefu kwani sehemu nyingi walizopakana nazo zimepata umeme lakini wenyewe walitelekezwa.

"Hatujapata mbunge mwenye kasi kama hii ya kutusaidia kupata umeme hivyo tunaamini kuwa maendeleo yafakuja kwa kasi," alisema Hussein.


Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: