Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula kujengea uwezo  vikundi 375 vya ujasirimali, ikiwa vikundi 182 ni vikundi vipya vilivyosajiriwa kwa msaada wa uratibu wa Ofisi ya Mbunge na kugharimu takribani shilingi  12,740,000 za kitanzania, ikiwa ni fedha ya usajiri, Kitabu cha Bank, na mchakato wa uandaaji wa Katiba.

Haya yamebainishwa na katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana Ndg Heri Nkoromo maarufu Kipara katika Kongamano la Uchumi, Uwekezaji na Mahusiano lilobeba jina la" Red and Silver Party" na kuratibiwa na kikundi cha "Mwanamke Mpambanaji"  lilofanyika JB Belment ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula.

Ndg Kipara ametumia adhara hiyo kusema, Mhe Mabula kupitia ofisi yake kwa ushirikiano na Taasis ya First Community Organisation imeweka mkakati wa kuvifikia vikundi 375 katika  mafunzo ya ujasirimali na stadi za kazi. Mafunzo yatakayoanza karibuni kwa makundi ya Vijana, Wanawake na Wajasirimali.

Mafunzo haya yatagusa nyanja mbali za ujasirimali ikiwa ni pamoja na Uandikaji wa Andiko mradi, biashara na masoko, usindikaji wa Maziwa, utengenezaji wa Sabuni, Batiki sanjari na Ufugaji wa kisasa ma Kuku na Ng'ombe pamoja na Nguruwe. Na miongoni mwa Vikundi vitakavyo nufaika ni Vikundi vya Vijana na Wanawake kikiwemo kikundi cha Mwanamke Mpambanaji ili kunufaika na tengo la fedha 10% ya halmshauri Jiji la Mwanza.

Naye katibu wa kikundi cha 'Mwanamke Mpambanaji' akisoma risala amesema kikundi hicho kilianzishwa mwanzo mwa Mwaka 2018 na tarehe 1.6.2018 kilipata usajiri rasmi dhima kuu ikiwa ni Kutoa uhamasishaji wa shughuli za Uchumi na maendeleo kwa Wanawake na Mabinti pamoja na utoaji wa mikopo ya riba nafuu.

Kogamano hili kubwa limekuwa la kwanza kuandaliwa na kikundi Mwanamke Mpambanaji na kuhusisha  wasanii wa kizazi kipya,  wakufunzi wa kitaifa na kimataifa katika Biashara na uchumi,  pychologist, mahusiano pamoja na chakula cha Usiku.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana 🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: