Tuesday, 7 August 2018

Hakikisheni Taarifa Mnazozitoa Wakati Wa Kusajili Kadi Zenu Za Simu Ni Sahihi, Vinginevyo Sheria Itafuata Mkondo Wake

Na. Vero Ignatus Arusha.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imewataka wananchi kufahamu wajibu na haki zao wanazostahili  kupata kutoka kwenye mitandao inayotoa  huduma za mawasiliano sambamba na kutambua wajibu walionao kama watumiaji wa huduma za mawasiliano

Kaimu mkuu wa Kanda ya kaskazini Francis  Msungu amesema kuwa mamlaka inatoa elimu kwa wananchi kuzijua haki zao kutokana na mabadiliko yanayotokea ni mengi ya sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo ya matumizi ya vifaa vya mawasiliano katika mitandao ya simu.

Amesema kwa sasa kumezuka wimbi la utapeli kupitia simu za mikononi,  hivyo wananchi  wametakiwa kuwa na tahadhari kubwa, wasikubali kurubuniwa katika vitu ambavyowanafahamuhawajashiriki Usitekeleze maagizo yeyote yahusuyo fedha kwa ujumbe wa maandishi,

"Mfano unatumiwa ujumbe kuwa umeshinda bahati na sibu katika
Mashindano ambayo hujashiriki, ukipokea ujumbe umetumiwa pesa na mtu usiyemfahamu usizitoe fedha hizo, hadi uthibitishe ya kwamba zimetumwa kwa nia nzuri"

Amewataka wananchi mara waonapo fedha imetumwa kwenye mitandao yao  na aliyezituma bado hajafahamika, ni vyema wakawa na subira hadi watakapo hakikisha zimetumwa kwa nia njema ili wasiingie kwenye matatizo.

"Watu huwa wanakosea pia yamkini zilitumwa kwa bahati mbaya, ukiwahi kuzitoa nawe unahesabika unaiba. "alisema

Amewataka watumiaji wa simu za mkononi kufahamu kuwa zipo tahadhari za kuchukuliwa ikiwepo kusajili namba kwa majina kamili  ya muhusika kwani ni takwa la kisheria, bila kusahau kwamba kila taarifa zinazoyolewa wakati wa usajili ziwe za sahihi.

Taarifa zako zikiwa za uongo hilo nikosa kisheria utapata adhabu ya kifungo au kulipa shilingi milioni 3 au vyote kwa pamoja.

Ameshauri kwamba yeyote akipoteza simu au kadi atoe taarifa kwa jeshi la polisi na kwa mtoa huduma, samba na kuchukua tahadhari mara uokotapo simu au kadi ya simu utoe taarifa kwa usalama wako zaidi

Wananchi wote wanaotembelea maonyesho  25 ya kilimo na sherehe za nanenane kanda ya kaskazini mwaka 2018 wanashauriwa kutembelea banda la TCRA ili waweze kupata elimu zaidi ya mawasiliano.

No comments:

Post a comment