Thursday, 23 August 2018

Dc jerry muro amkaribisha mkurugenzi mpya wa Meru


Mkuu wa Wilaya ya Meru Jerry Muro amemkaribisha Mkurugenzi Mpya wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Emmanuel Mkongo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Nd. Emmanuel Mkongo aripoti rasmi kwenye Halmashauri hiyo tayari kuanza uteelezaji wa majukumu yake.

Mkurugenzi Mkongo amewasili ofisini  baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 13 Agosti 2017 .

Mkurugenzi Mkongo amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro pamoja na kaimu Mkurugenzi ambaye ni mkuu wa idara ya utawala na rasilimali watu Grace Mbilinyi
Mkurugenzi Mkongo wakati wa kikao cha kufahamiana na wakuu wa idara na vitengo ,aliweka bayana dira ya uongozi wake ni kuisimamia vyema Halmashauri hiyo kwa mujibu wa sheria na kujikita kwenye ukusanyaji wa mapato yatakayotumika kuiendesha Halmashauri hiyo na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mkongo amewaasa wakuu hao wa idara na vitengo kufanya kazi kwa ushirikiano na kutekeleza majukumu yao ipasavyo pamoja na kuwasimamia vyema watumishi walio chini yao sambamba na kuzingatia taaluma zao kutoa ushauri utakaoleta tija katika Halmashauri hiyo .“sitegemei kupewa taarifa isiyo sahihi na afisa wa Halmashauri hii” amesisitiza Mkongo.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa idara na Vitengo Afisa elimu wa Sekondari, Mwl. Damari Mchome amempongeza Mkurugenzi Mkongo kwa kuteuliwa, pia ameeleza wapo tayari kumpa ushirikiano .

Kabla ya uteuzi wa Mkurugenzi Emmanuel Mkongo Halmashauri ya Wilaya ya Meru ilikuwa inaongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi Ndg. Christopher Kazeri.

No comments:

Post a comment