Waziri Jafo: Serikali Ya Magufuli “Sio ya walimila Dole”. - MSUMBA NEWS BLOG

Monday, 23 July 2018

Waziri Jafo: Serikali Ya Magufuli “Sio ya walimila Dole”.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo jana alitembelea halmashauri ya wilaya ya Kibaha kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

 Katika Ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea kituo cha afya Mlandizi, ukarabati wa sekondari ya wasichana ya Ruvu, pamoja na uboreshaji wa Kituo cha afya cha Magindu ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.9 zimeshatolewa na serikali kufanikisha miradi hiyo.

 Akizungumza na wananchi wa Magindu waziri Jafo aliwaambia wananchi hao kwamba serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli ni serikali ya vitendo sio ya kuahidi bila kutekeleza na kwamba kwa kizaramo “Sio ya walimila Dole”.

 Jafo alitumia neno hilo la Lugha ya kizaramo kwa wakazi hao wa magindu ambao wengi wao ni wazaramo ili kuleta msisitizo.

 Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamood Abuu Jumaa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kiwaletea wananchi wa kibaha vijijini maendeleo ya kweli.

 Aidha, waziri Jafo amewapongeza viongozi wa Kibaha vijijini kwa usimamizi mzuri wa ukarabati wa shule ya Ruvu kwani kwasasa imekuwa shule ya kuvutia kutokana na usimamizi mzuri wa fedha za serikali.

Hata hivyo katika ziara hiyo, Jafo ametoa mwezi mmoja agizo la kuwekwa majokofu jengo la kuhifadhia maiti katika kituo cha afya mlandizi lililojengwa tangu mwaka 2015 ili  wananchi waweze kupata huduma hiyo.

 Nao, wananchi wa Magindu wamemshukuru mbunge wao kwa kuwapigania mpaka wamepatiwa fedha hizo za maendeleo.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done