Friday, 6 July 2018

Watu Watano wafariki kwa Ajali Mbeya

Usiku wa kuamkia leo kumetokea ajali mkoani Mbeya katika eneo la Uyole ambapo Lori limegongana na gari ya Coca na kuilalia gari ingine aina ya Noah.
Ajali hiyo imehusisha magari matatu imetokea kwenye mteremko wa mlima Igawilo na kwa mujibu wa mashuhuda gari lenye kontena limeliangukia gari aina ya Noah iliyokuwa na abiria na inasadikiwa watu wanne wamepoteza maisha.
Ajali hii imetokea ikiwa ni saa chache baada ya Waziri Mpya wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kutembelea Mbeya na kutangaza kuvunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani pamoja na Kamati zake zote za Mikoa na Wilaya

No comments:

Post a Comment