Thursday, 12 July 2018

Tigo Yazindua Kampeni mpya ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa

Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imezindua kampeni ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’, kama uthibitisho kuwa huduma hiyo sasa ina hadhi ya huduma kamili ya kifedha ambayo inawapa wateja huduma za kipekee, bora na  nyingi zaidi kupitia mtandao wa simu. 

‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’ inazingatia sifa ya Tigo kuwa mtandao pekee unaobuni huduma na bidhaa kulingana na mahitaji ya wateja ili kuboresha na kurahisisha maisha yao. 

‘Tigo Pesa imepanua wigo wa bidhaa na huduma zake na kuibua njia bora zaidi kwa wateja kufurahia huduma za haraka, uhakika na salama za kifedha popote walipo nchini Tanzania,’ Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa  Huduma za Kifedha wa Tigo aliwaambia waandishi wa habari. 

Kama sehemu ya kampeni hii, Tigo Pesa inajivunia kuwa mtandao pekee na wa kwanza wa simu unaotoa huduma inayowezesha wateja wa Tigo kurudisha miamala ya fedha zilizotumwa kimakosa kwenda kwa wateja wenzao wa Tigo.  Huduma hiyo inayopatikana kupitia menu ya Tigo Pesa  *150*01# inawapa wateja wa Tigo uwezo wa kurudisha kwa haraka miamala yoyote ya kutuma hela ikiwa watagundua kuwa wamekosea miamala hiyo, bila ya kuhitaji msaada wa moja kwa moja kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. 

‘Huduma hii ya kipekee ya kurudisha miamala iliyokosewa kwa haraka inajibu mahitaji ya wateja wengi ambao kwa sababu moja au nyingine wanafanya makosa pindi wanapotuma pesa. Ni huduma ya aina yake ambayo inawapa wateja uwezo zaidi juu ya miamala wanayofanya na imeundwa kwa kuzingatia vigezo vya hali ya juu vitakavyozuia matumizi mabaya ya huduma hii,’ Hussein alifafanua
Afisa Mkuu wa  Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa.’ Tigo Pesa pia imezindua huduma mpya ya Jihudumie itakayowasaidia wateja wa Tigo kurudisha miamala ya kutuma fedha waliyokosea, bila kuhitaji msaada kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. Kulia ni Mkuu wa Udhibiti Ubora wa Tigo Pesa, Angelica Pesha.

No comments:

Post a Comment