Tuesday, 10 July 2018

OPERESHENI ENDELEVU YA UKAGUZI WA MGARI USIKU NA MCHANA ARUSHA YAPAMBA MOTO

 Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'anzi akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo kikuu cha polisi Arusha,aliyepo kulia kwake ni Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Arusha Joseph Bukombe.Picha na Vero Ignatus.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Arusha Joseph Bukombe akionyesha moja ya makosa waliyoyabaini baada ya kufanya ukaguzi kwenye moja ya Lori la kubebea mizigo.Picha na Vero Ignatus.
 Baadhi ya pikipiki zilizokamatwa zikiwa katika kituo kikuu cha polisi mkoani Arusha.

Haya ni baadhi ya magari ya kubebea mizigo yaliyokamatwa na makosa tofauti tofauti.Pichq na Vero Ignatus.
 Mkaguzi wa Magari kutoka kikosi cha usalama barabarani akionyesha jinsi ambavyo gari kwa nje linaonekana jipya lakini kwa ndani lina ubovu,kama inavyoonekana  katika picha chuma kikiwa kimevungwa na mfuko wa kiroba .
 Basi la Abiria kampuni ya Chakito amabalo linashikiliwa kituoni hapo kwa ubovu,taa zote haziwaki,kioo cha kuangalia usalama sitemirrow kimefungwa kwa manati pamoja na makosa mengine mengi.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Ni operesheni endelevu yakukagua magari na pikipiki yenye makosa mbalimbali ya usalama barabarani mkoani Arusha ambapo jumla ya magari 1719 yalikaguliwa pikipiki 182,madereva 189 walipimwa ulevi na dereva mmoja wa basi alikutwa na kilevi anashikiliwa na jeshi la polisi.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Ramadhani Ng'anzi amesema jumla ya makosa mbalimbali ya usalama barabarani yaliyokamatwa kuanzia tarehe 07.07 hadi 09.07.2018 ni 1901 na jumla ya tozo na notification zilizokusanywa kwa kipindi hicho ni shilingi milioni hamsini na saba na thelatini elfu.(57,030,000)

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe amesema mabasi ya abiria 102 yalikaguliwa kati ya hayo 7 yalikutwa mabovu ambapo yalizuiliwa yasiendelee na safari sambamba na malori  129 kati ya hayo 16 yamng'olewa namba kwa ubovu ili wamiliki wa magari hayo wakayatengeneze.

Kwasababu mtu anaweza kwenda shimoni huko akarudi jionihiyo siyo issue,kari ni zima?inakiwango?dereva anayeendesha anasifa ya kuendesha!ndiyo kitu amabacho tunakitaka"alisisitiza RTO

 Amesema wameamua kufanya oparesheni hiyo usiku na mchana kwani madereva hao wanapaki magari mchana usiku wanayaweka barabarani kuendekea na shughuli kama kawaida.

"Tumeamua kufanya oparesheni hii mchana hayaonekani wanapaki kwahiyo usiku ndiyo tunafanya ili tuwapate " alisema Bukombe.

Jumla ya pikipiki 161 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani na kuandikiwa faini ,leseni 365 zilikaguliwa kati ya hizo 104 zimekwisha muda wake.

 RTO Arusha Joseph Bukombe akionyesha moja ya lori la mchanga ambalo halina reflector na mara nyingi yanafanya kazi usiku.Picha na Vero Ignatus.
Wakaguzi wa magari (vehicle inspectors) wakiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe na baadhi ya waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus.


No comments:

Post a Comment