Mbunge wa Iramba Magharibi,  Dk Mwigulu Nchemba amewataka wakazi wa jimbo hilo kutosikiliza maneno ya watu wanaosema kuwa anaweza kujiuzlu nafasi ya ubunge baada ya kuondolewa katika baraza la mawaziri.

Dk Mwigulu alitoa kauli wakati akiwa kwenye mkutano na wakazi Kata ya Ulemo kijiji cha Misigiri wilayani Iramba mkoani Singida.

Alisema uongozi ni kupokezana kijiti na kwamba si kweli kwamba analengo la kuacha nafasi hiyo na kwamba ataendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa mda wote tofauti na mwanzo alivyokuwa kwenye majukumu ya kitaifa.

Alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais John Magufuli kwa kumwamini na kumpa na nafasi katika serikali yake hadi alipombadilisha na hana kinyongo chochote,  ataendelea kufanya kazi chini ya mwenyekiti wa CCM na serikali pale itakapoitajika huduma yake.

Alifafanua kuwa uliona wapi mchezaji akasajiliwa kwenye klabu yake, kisha akaitwa timu ya taifa na siku akiondoka timu ya taifa anasema klabu yenu siichezei.

“Hao wanaosema nataka kujiuzulu ubunge, wanataka kutengeneza jambo la ugomvi. lakini kwangu sioni kama ni ugomvi wala tatizo nimerudi kuwatumikia wananchi wa jimbo kwa kazi mlionituma
Share To:

msumbanews

Post A Comment: