Tuesday, 10 July 2018

Mke wa Alikiba, Bi Amina ni mjamzito?

Huwenda ndoa ya Alikiba na mke wake Bi. Amina Rikesh iliyofungwa mapema mwaka huu ikawa imezaa matunda kwani tetesi zilizopo mitandaoni ni kwamba binti huyo ni mjamzito.

Wiki hii ilikuwa ni birthday ya Seven Mosha meneja wa muimbaji Alikiba ambapo wanafamilia wote wa RockStars 4000 walionekana katika picha ya pamoja inayodaiwa kupigwa nchini Afrika Kusini.
Kama wadau wa mambo wanavyosema, picha moja ni sawa na maneno 1000. Hivyo hivyo kwenye picha aliyoipost Alikiba akiwa mke wake, Bi. Amina, meneja wake Seven Mosha pamoja na marafiki zake wengine.
Kwani licha ya kuandika ujumbe huu “With the Birthday Girl @sevenmosha
#mofayabyalikiba #KingKiba” kupitia picha hiyo. Lakini mashabiki wameenda mbali zaidi kwa kudai kwamba picha hiyo inamuonyesha mwanadada huyo akiwa ana hali ya ujauzito.
Hebu na wewe angalia picha hapo juu na utoe maoni yako. Hizi hapa chini ni baadhi ya komenti za mashabiki wa Instagram baada ya kuona picha hiyo.
Didalitow
Kama vile wifi anakibend😯😯😯
Naahassan
Maashallah Mabrouk Ali kiba na mkeo tunatarajia aunty soon.
Mzomoziallan
King naona ushatupia hapo.

No comments:

Post a Comment