Sunday, 22 July 2018

Mh: Amina Mollel Aongoza mahafali ya Kidato cha Sita


Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Arusha Mh: Amina Mollel amewataka wahitimu wa Kidato cha sita  kujiadhari na ugonjwa wa ukimwi wafikapo ndani ya yuo kwani wakasome kwa bidii na sio vinginevyo.

Wito  huo ameutoa katika mahafali ya kwanza ya Kidato cha sita  katika Shule ya Mlangarini iliyopo wilayani Atumeru  Jana ambapo alikuwa mgeni Rasmi.

"Ni wasihi tu mkipokea mikopo hizo fedha zisiwe moto kwenu kuwaunguza Bali ziwe njia kuu ya kuwawezesha kusoma kwa bidii na sio vinginevyo, mkajiadhari na ugonjwa wa ukimwi maana vyuoni  hamuendi kulindwa tena  bila kujilinda mwenyewe hutoweza kufikisha malengo yako"

Pia muheshimiwa mbunge aliwasihi wazazi kuwatoa watoto wao wakike kwa kuwapeleka Shule na sio kuwaozesha.

Sambamba na hapo mh: Amina Mollel aliwataka wanafunzi wa vidato vingine kuiga mfano wa Shule ya Kisimiri ili mwakani waweze kuongoza katika Matokeo ya Kidato cha NNE na cha sita.
Mbunge wa Viti Maalum Mh. Amina Mollel Akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc  Dr. Wilson Mahera.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc Dr. Wilson Mahera Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari Mlangarini.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlangarini wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi.


  • Walimu wa Shule ya Mlangarini wakimsikiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc Dr. Wilson Mahera

No comments:

Post a comment