Mh: Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana amebanisha katika alipokuwa anazungumza na Ndg Sitta Tuma mwakilishi wa kanda wa taasi ya Free Media Group Company LMT inayomiliki magazeti ya Tanzania Daima na Sayari  katika ziara yake kwenye taasi za habari kwa siku tatu. 

Mhe Mabula akijibu swali kutoka kwa mwakilishi wa Kanda Sitta Tuma  lililo hoji ni mkakati  gani Mbunge anao katika kusaidia upatikanaji rahisi wa taarifa za miradi ya maendeleo.

Mhe Mabula amesema mbali na kuwa na tovuti ya halmashauri ya Jiji la Mwanza kadharika ofisi yake tayari inandaa mfumo rahisi na shirikishi utakaowezesha upatikanaji wa taarifa za miradi ya maendeleo pamoja utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi  wakati wowote kwanzia ngazi ya mtaa, mitandao ya jamii, tovuti, jarida pamoja na vyombo vya habari.

Mhe Mabula amefafanua kuwa wananchi wamekuwa makini kufuatilia miradi ya maendeleo kwa kuwa serikali ya CCM imerejesha dhana ya uwazi na uwajibikaji kwa miradi ya maendeleo kwanzia mchakato ya zabuni hadi utoaji zabuni na utekelezaji wake kuwa wazi katika ngazi husika na michakato yake ni wazi hadi mradi utakapo kamilika.

Mhe Mabula pia amepongeza taasis hiyo kuwa wadau wakubwa katika kutoa taarifa za Mbunge wa Nyamagana anayetokana na CCM hata kama Mmiliki wa taasis hiyo nikutokea Chama Cha Upinzani.  Ziara hii ya Mhe Mabula  katika Vyombo Vya habari  imeanza  leo tarehe 16.07.2018 na itaisha kesho kutwa Ijumatano tarehe 18.07.2018.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: