Jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kushirikiana na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) wamekamata na kuteketeza mashine feki 45 za michezo ya kubahatisha zilizoingizwa nchini kinyemela.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Julai 26, 2018 kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'anzi amesema  mashine hizo zilikatwa maeneo mbalimbali  jijini hapa  katika operesheni iliyofanyika kwa kipindi cha wiki moja.

Amesema katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wawili akiwemo raia mmoja wa China.

Amesema wamebaini  mashine hazikusajiliwa kutumika  nchini na hazikulipiwa kodi na zilikuwa zikitumika katika maeneo ambayo hayajaidhinishwa na bodi hiyo.

Meneja wa ukaguzi na udhibiti wa bodi hiyo, Sadick Elimsu amesema  awali bodi hiyo ilipata taarifa za kuingizwa kinyemela kwa mashine hizo bila kufuata utaratibu wa usajili huku baadhi yake zikiwa ni feki.

Amesema mashine hizo zimesambazwa katika maeneo mbalimbali yasiyoidhinishwa na zinatumika kuwaibia wananchi na zimekuwa zikiendeshwa bila kulipia kodi ya Serikali.

Amesema operesheni inaendelea katika maeneo mbalimbali nchini na  hivi karibuni mkoani Kigoma walikamata na kuteketeza mashine zaidi ya 80.

Katika hatua nyingine polisi  mkoa wa Arusha wanawashikilia watu 40 kwa tuhuma mbalimbali ya uhalifu; wanane kwa tuhuma za kukutwa na misokoto 18 ya bangi pamoja na madereva 20 wa malori ya mchanga, wakitumiwa kutumiwa magari mabovu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: