Sunday, 8 July 2018

Majaliwa awataka Tizeba, Ndalichako kukutana kujadili kukuza uchumi


Na James Timber, Mwanza
Serikali imemuagiza  Waziri wa Kilimo Charles Tizeba na Waziri wa elimu Joyce Ndalichako kukutana ili kujadili namna ya kushirikiana katika kukuza uchumi kwa wananchi.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kilele cha Maadhimisho ya Ushirika Duniani ambapo Kitaifa yamefanyika jijini Mwanza na kusema kuwa wizara hizo zitasaidia kuboresha maisha ya wananchi hasa wakulima.

Aidha Majaliwa amesema changamoto kubwa inayokabili vyama vya ushirika ni wizi, ubadhilifu wa mali za ushirika jambo linalofanya wananchi kutokuwa na imani na vyama hivyo.

Pia Majaliwa amewataka maafisa Ushirika waliopo wilayani wanatakiwa kusimamia vyama vya ushirika katika maeneo yao ili wananchi waweze kunufaika na ushirika huo.

No comments:

Post a Comment