Sunday, 8 July 2018

ILALA YAKABIDHI MWENGE WA MWENGE WA UHURU KIGAMBONI

 Wilaya Ilala leo imekabidhi Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Kigamboni baada ya kutembelea na kuzindua miradi ya maendeleo ipatayo sita, yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 4. 3.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyo fanyika katika uwanja wa Shababi uliko katika kata ya Tungi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemshukuru kiongozi wa mbio za Mwenge Charles Kabeho kwa kuzindua miradi  hiyo na kusema kuwa Ilala imejipanga katika kusimamia fedha za selikali  ili kupata thamani halisi ya fedha kulingana na mradi husika.


 Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge Charles Kabeho ameipongeza Manispaa ya Ilala kwa  kwa miradi yake ambayo imezingatia viwango nakusema kuwa ameitisha  yote baada ya kufanya ukaguzi wa kina na kujiridhisha kuwa  miradi hiyo imeenda na viwango na thamani halisi ya fedha.No comments:

Post a Comment