Thursday, 12 July 2018

Hamissa Mobetto na Ray C Ndani ya Bifu Zito

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amejikuta katikati ya bifu zito na mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto.

Sintofahamu hiyo Ilianza siku mbili nyuma baada ya Ray C kuzisema nguo aina ya‘Fendi’ ni feki ambazo zimekuwa zikiuzwa sana na Hamisa ambaye ni mfanyabiashara ambapo Ray C alitoa kama maneno ya kejeli kuhusu nguo hizo ingawa hakutaja jina.
Basi Hamisa baada ya kuona kama Dongo lile katupiwa yeye basi moja kwa moja akaandika ujumbe ambao uliwakosoa watu ambao hawaonyeshi sapoti kwa biashara za wengine badala yake wanakuwa na wivu.
Baada ya sakata hilo na mashabiki wa Hamisa kumvamia Ray C basi aliweka wazi kuwa hakumtaja Hamisa jina kwa lile Dongo lakini baada ya kuona wanazidi ikabidi amvae Hamisa na kumsema kuhusu Zari na kudai yeye mwenyewe alimuumiza Zari kwa kitendo cha kuzaa na Diamond.

No comments:

Post a comment