Wednesday, 18 July 2018

Gari la Halmashauri ya Babati lapata Ajali wawili wafariki Dunia


Watu wawili wanadhaniwa kufariki dunia na wawili kujeruhiwa vibaya baada ya Malori mawili kugongana usiku huu katika eneo la Logia Mjini Babati Mkoani Manyara.

Taarifa ambazo Msumbanews.co.tz Imezipata zinaeleza kuwa Dereva wa Gari ya Halmashauri alikuwa akijaribu kulipita Lori lililokuwa mbele yake ndipo alipofeli na kugonga kwa nyuma na kupelea vifo hivyo.

Majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Dareda Mission kwa matibabu, Eneo lilipotokea ajali licha ya kuwekwa tahadhari kutokana na miteremko na kona kali lakini bado madereva hawazingatii alama hizo.

No comments:

Post a comment