Wednesday, 18 July 2018

Baada ya Makonda kupata mtoto Wema, Diamond watoa neno

 STAA wa Bongo Fleva Diamond Platinumz na aliyewahi kuwa mpenzi wake ambaye pia ni Malkia wa Bongo movies, Wema Sepetu wametoa neno la pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mkewe kwa kufanikiwa kupata mtoto wa kiume waliyompa jina la Keagan.

“Keagan ni mtoto atakaependwa sana wallahy, yaani uwiiii simpatii picha, Keagan you are a blessing to your Mummy and Daddy, and with parents like yours I guarantee you are going to be a good Boy, a blessed child,” ameandika Wema.

 Ambwene Yessaya “AY” hakuwa nyuma, naye ametupia ujumbe huu kwa Makonda na mkewe;

“Hongereni sana Familia ya Paul Makonda kwa kupata mtoto. Mungu awajaalie Baraka na Upendo na awasimamie katika malezi ya mtoto.”
 Diamond naye akafunguka;

“Congrats, Paul Makonda, Mwenyezi Mungu amkuze mtoto vyema na kumkinga na mabaya ya walimwengu.
Kupitia kurasa zao za Instagram, Wema ameandika maneno haya kwa Makonda;

“Hakika kuna Mungu, wakati wa Mungu ndo wakati sahihi, hongera sana kaka yangu na wifi yangu, kama nawaona, mtoto raha jamani, congratulations once again. All these testimonies are giving me sooo much hope. Tuseme Inshallah, congrats Baba na Mama Keagan.

No comments:

Post a comment