Monday, 2 July 2018

Atomiki washiriki maonesho ya Sabasaba kuonyesha ushirikiano wa URT na Shirika la Nguvu za Atomiki DunianiUmoja wa Mataifa (UN) kupitia Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaojulikana kama UNDAPII  umekuwa ukitoa ushirikiano mkubwa wa maendeleo nchini Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya nchi yetu kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa na Serikali ili nchi iweze kufikia malengo.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ambaye ndiye mratibu na msimamizi wa miradi mingi ya Teknolojia  ya Nyuklia inayotekelezwa hapa nchini hususani katika sekta za Afya, Kilimo, Nishati,Viwanda, Ujenzi, na Maji,  kupitia ufadhili Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) ambalo liko chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa, inashiriki kwenye Maonesho ya SabaSaba yaliyoanza tarehe 28 Julai, 2018 ili kuonyesha utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa pamoja (Derivering as One) ili kufikia Malengo ya Dunia.
Tunapatika kwenye banda la UN No. 181 Jengo la Karume katika kipindi chote cha Maonesho ya Saba Saba

“Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa”

Imetolewa na;

Peter G. Ngamilo
Afisa Mawasiliano Mwandamizi
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

No comments:

Post a comment