Thursday, 7 June 2018

Wasanii 6 kutoka BSS wanaofanya vizuri, kwa mujibu wa Madam Rita

Chief Judge wa Shindano la Bongo Star Search (BSS), Madam Rita Paulsen ametaja wasanii sita kutoka kwenye shindano hilo ambao kwa sasa wanafanya vizuri.
Madam Rita amesema si kweli wasanii kutoka BSS hawafanyi vizuri ila wanafanya kwa namna nyingine kutokana na siasa zilizopo kwenye muziki wa Bongo Flava kwa sasa.
Wasanii aliowataja kufanya vizuri ni pamoja na Walter Chilambo, Peter Msechu, Kala Jeremiah, Haji Ramadhani, Frida Amani na Angel Kato.
“Wapo wengi wanafanya vizuri, wapo kama Walter Chilambo yupo kwenye gospel kama wewe si mtu wa gospel utajuaje kama ni big star. Kuna wengine wapo kwenye mabendi, Haji Ramadhani ni mtu muhimu kwenye Twanga Pepeta, kuna Peter Msechu, Kala Jeremiah,” amesema.
“Kuna ma-presenter wa radio, Frida Amani wimbo wake kwa sasa unafanya vizuri kila mahali, Angel Mary wanafanya vizuri,” Madam Rita ameiambia Wasafi TV.
Madam Rita Paulsen amesisitiza kuwa wote hao wanafanya vizuri ila inategemea anayewatazama anataka awasikie wapi wakifanya vizuri ila anachojali si wao kusikika tu bali ni kuona na maisha yao yamebadilika kitu ambacho wamefanikiwa.

No comments:

Post a Comment