Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa ahirisho la mwisho kwa upande wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa sababu wameshindwa kufika na shahidi.

Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita kudai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Wakili Mwita amedai kuwa hawana shahidi na kwamba hiyo ni mara ya tatu hawana shahidi, hivyo wanaomba ahirisho.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba amesema anatoa ahirisho la mwisho kwa upande wa mashtaka, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi June 29,2018.

Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa kuwa alifanya kosa hilo July 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.

Anadaiwa  kumtukana Rais John Magufuli  kuwa “anaongea hovyohovyo, anatakiwa  afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa Amani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: